Back

ⓘ Cheo
                                               

Kaizari

Asili ya cheo ni Julius Caesar aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka 44 KK. Watawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar kwa heshima yake hadi jina likawa cheo. Cheo cha Kaizari kiliendelea kutumika katika eneo la Dola la Roma ya Mashariki Bizanti hadi mwaka 1453.

                                               

Sultani

Neno lenyewe lamaanisha "nguvu", "mamlaka" au "utawala" likawa baadaye kama cheo cha mtawala wa kiislamu mwenye kujitegemea bila kuwa na mwingine juu yake.

                                               

Papa

Kwa samaki anayeitwa kwa Kiswahili "papa" tazama papa samaki Papa ni cheo cha kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote. Cheo hicho kinategemea kile cha askofu wa Roma.

                                               

Askofu

Neno episkopos linaonekana kama cheo katika maandishi ya mwisho wa karne I na mwanzo wa karne II kama vile waraka wa kwanza wa Klementi ambapo askofu aonekana kuwa kiongozi mkuu wa kanisa la mji fulani. Katika uenezi wa Ukristo madaraka ya askofu yalipanuka. Kadiri makanisa yalivyoenea hata nje ya miji hadi mashambani askofu akawa kiongozi wa eneo, si wa mji tu. Wakati ule ngazi za daraja zilionekana: Kanisa la mji au eneo likiongozwa na episkopos askofu akishauriana na "presbiteri" kiasili: wazee; baadaye: makasisi na kusaidiwa na mashemasi au madikoni.

                                               

Askofu mkuu

Askofu mkuu ni cheo cha askofu kiongozi anayesimamia maaskofu katika jimbo la kanisa lenye dayosisi mbalimbali. Asili ya neno lenyewe ni Kigiriki αρχή arché mwanzo, wa kwanza. Sehemu ya pili ni neno la Kigiriki επίσκοπος episkopos mwangalizi lililofikia Kiswahili kupitia umbo la Kiarabu uskuf.

                                               

Gavana

Kuna nchi ambako gavana ni mtendaji mkuu wa serikali katika dola la shirikisho au jimbo. Kwa mfano katika Marekani ina madola 50 ndani yake na kila moja huwa na gavana kama mkuu wa serikali ya kidola. Cheo hiki kinalingana na waziri mkuu wa sehemu ya nchi yenye kiwango cha kujitawala na bunge lake pamoja na serikali ya kieneo, kwa mfano waziri mkuu wa jimbo la Afrika Kusini au Ujerumani.

                                               

Khalifa

Khalifa ni cheo cha kihistoria kwa ajili ya kiongozi wa ummah. Ni neno la Kiarabu خليفة khalīfah linalomaanisha "makamu". Khalifa ni kifupi chake cha خليفة رسول الله "khalifatu-rasul-i-llah" kinachomaanisha "Makamu wa mtume wa Allah/Mungu". Hivyo mana yake ni makamu au mfuasi wa Mtume Muhammad katika nafasi yake kama kiongozi wa Waislamu. Cheo cha khalifa kilitumiwa pamoja na cheo cha amīr-al-muminīn أمير المؤمنين "Jemadari Mkuu wa wenye Imani =Waislamu". Utaratibu wa uongozi wa khalifa ulianzishwa baada ya kifo cha Muhammad mw. 632 na kuishia 3 Machi 1924 katika mapinduzi ya Atatürk.

                                               

Amiri

Amiri au Emir ni cheo cha mtawala mwislamu anayesimamia emirati. Kiasili maana yake ni "mwenye amri" kama cheo cha kijeshi au kiserikali. Katika miaka ya kwanza ya Uislamu amiri alikuwa mkuu wa jeshi au sehemu ya jeshi. Baada ya kutwaa nchi alikuwa na nafasi kama gavana ya khalifa. Kutokana na upanuzi wa himaya ya kiislamu na ushaifu wa serikali kuu amiri aliweza kutawala mara nyingi kama mfalme mdogo lakini kwa kawaida alitafuta kibali cha khalifa.

                                               

Mfalme

Mfalme ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingine hasa kama mfalme aliyetangulia alikufa bila mrithi. Utawala wa kifalme ilikuwa hali ya kawaida katika nchi nyingi za dunia kwa muda mrefu. Mwanamke anayeshika nafasi ya mfalme huitwa "malkia". Kama cheo kinaendelea katika ukoo mmoja kutoka mababa kwa watoto wao familia hii huitwa nasaba.

                                               

Kapteni

Kapteni ni cheo cha kijeshi katika nchi nyingi za dunia. Kapteni huwa ni kiongozi wa kikosi cha askari 100-200. Madaraka ya kapteni ni kuongoza kikosi chake akisaidiwa na maluteni wake. Kwa kawaida hatashiriki katika mipango ya vita bali wajibu wake ni kutekeleza maagizo ya wakubwa wake. Katika jeshi la wanamaji kapteni captain hutokea kama cheo cha kiongozi wa manowari kwa hiyo kuna uwezekano ya kwamba kapteni huyu ana madaraka zaidi kuliko kapteni kwenye nchi kavu. Neno limeingia katika Kiswahili kutoka lugha ya Kiingereza. Asili ya cheo ni neno la Kilatini "caput" linalomaanisha "kichwa ...

                                               

Tsar

Tsar ilikuwa cheo cha mfalme au mfalme mkuu katika Urusi na pia katika Serbia na Bulgaria. Asili ya neno ni Julius Caesar aliyekuwa kiongozi wa Dola la Roma hadi kuuawa kwake na wapinzani mwaka 44 KK. Watawala waliomfuata walianza kutumia jina la Caesar kwa heshima yake hadi jina lilikuwa cheo. Cheo cha "Caesar" likawa "kaisar" kwa lugha ya Kigiriki na kuingia katika lugha za nchi zilizojaribu kuendeleza Dola la Roma: "Kaiser" wa Dola Takatifu la Kiroma Ujerumani aliyeingia katika Kiswahili kama "kaizari". "Tsar" wa Urusi tangu 1453 baada ya mwisho wa Milki ya Bizanti iliyokuwa mabaki ya D ...

                                               

Abesi

Abesi ni cheo cha mmonaki wa kike anayeongoza monasteri kamili; kwa namna fulani kinalingana na kile cha abati.

                                               

Afande

Afande ni jina la heshima ambalo mwanajeshi au askari yeyote anamwita mkubwa wake. Inalingana na neno la Kiingereza "Sir" lililokuwa la kawaida katika jeshi wakati wa ukoloni wa Kiingereza.

                                               

Akida

Akida alikuwa mkubwa wa kikosi cha jeshi la zamani, kwa mfano la Dola la Roma. Katika Biblia ya Kikristo jina hilo linatumika kutafsiri neno la Kilatini "centurio", yaani mkuu wa askari mia. Maarufu zaidi ni yule ambaye alisimamia utekelezaji wa adhabu ya kifo kwa Yesu akamkiri kuwa kweli Mwana wa Mungu Mk 15:39, lakini pia yule aliyesifiwa na Yesu Kristo kwa imani yake kubwa Math 8:5-13: Lk 7:1-10, halafu akida Korneli aliyebatizwa kwa agizo la Mtume Petro bila kudaiwa kwanza atahiriwe Mdo 10:1-11:30.

                                               

Daktari

Daktari ni neno lenye asili ya Kilatini lililoingia Kiswahili kwa kupitia Kiingereza. Hutumiwa kwa maana mbili: 1) Mtaalamu aliyepata mafunzo maalum kwenye chuo kikuu cha kutibu maradhi ya wagonjwa. Mtu wenye ujuzi wa kutibu anaitwa pia mganga wa, tabibu ma. Daktari humtibu mgonjwa kwa kutumia sindano, kumtundikia dripu n.k. baada ya kumpima baadhi ya vitu kama: Kumpima mapigo ya moyo n.k. Maranyingi daktari hufanya kazi yake katika sehemu maalumu iitwayo Hospitali. Kumpima damu 2) Kwa kufuata tabia za lugha nyingine daktari hutumiwa pia kama jina la heshima kwa mtu aliyepata shahada ya uz ...

                                               

Daraja takatifu

Daraja takatifu katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo ni jina la vyeo vya askofu, kasisi na shemasi vinavyounda uongozi wa Kanisa. Katika Kanisa Katoliki na ya Waorthodoksi ngazi hizo tatu zinaunda kwa pamoja mojawapo ya sakramenti saba ambazo Yesu Kristo alizianzisha na kulikabidhi Kanisa lake. Baadhi ya Waprotestanti wana huduma hizo lakini kwao si sakramenti.

                                               

Kardinali mlinzi

Kardinali mlinzi alikuwa kardinali aliyeteuliwa na nchi, mashirika ya kitawa, vyama vya kitume, makanisa, mabweni na miji au aliyetolewa na Papa kwa miundo hiyo ili aisimamie kwa niaba yake na kuitetea huko Roma katika ofisi kuu za Kanisa Katoliki. Desturi hiyo ilianza katika karne ya 13 Fransisko wa Assisi alipomuomba papa Inosenti III na halafu papa Onori III apewe Ugolino, kardinali wa Ostia, kama mlinzi wa utawa wake wa Ndugu Wadogo. Mamlaka ya kardinali mlinzi iliongezwa au kupunguzwa kadiri ya mangamuzi mpaka iliposimamishwa kwa jumla baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano 1962-1965.

                                               

Khan

Khan ni cheo cha mtawala chenye asili kati ya wafugaji Wamongolia na Waturki wa Asia ya Kati. Mwanzoni kilikuwa cheo cha kijeshi kilichomaanisha Mkuu, amirijeshi au Bwana mkubwa. Baadaye ilimaanisha hasa mtawala. Kiasili cheo kilikuwa "khagan" lililofupishwa kuwa "khan" pekee. Wamongolia waliongozwa na Chingis Khan na kutokana na sifa zake matumizi ya cheo hiki kilisambaa pande nyingi za Asia. Madola mengi yaliyoongozwa na wasemaji wa Lugha za Kiturki yalitawaliwa na makhan au makhagan. Baadaye cheo hiki kilitumiwa pia kwa makabaila wa ngai za chbini zaidi. Leo hii "Khan" anayejulikana has ...

                                               

Kleri

Kleri ni kundi la watu wanaoongoza dini fulani. Jina linatokana na neno la Kigiriki "κλῆρος" - klēros, "bahati", "sudi" au also "urithi". Katika madhehebu mengi ya Ukristo kleri ina daraja takatifu tatu: kuanzia juu ni uaskofu, upadri na ushemasi. Hata hivyo baadhi yao wanapewa pia majina mengine kulingana na huduma zao, kwa mfano: Papa, kardinali, monsinyori, abati, kanoni, arkimandrita n.k. Katika Uislamu hakuna ukuhani, hivyo uongozi unategemea tu elimu ya dini: kuna mufti, imamu, ustadhi n.k.

                                               

Liwali

Asili ni neno la Kiarabu "الوالي" al-wali linalomaanisha mtawala wa mahali au eneo asiyejitegemea bali aliyeteuliwa na serikali kushughulikia mambo ya utawala katika eneo fulani. Mara nyingi katika nchi za utamaduni wa Uislamu Wali alisimamia "wilaya". Kazi yake ililingana na "gavana".

                                               

Luteni

Luteni, pia Luteni wa Kwanza, ni cheo cha afisa wa jeshi kilicho chini ya Kapteni na juu ya Luteni wa Pili. Asili ya neno ni Kifaransa lieu-tenant yaani "mwenye kushika nafasi" kwa maana ya naibu, makamu. Kiasili lieu-tenant alikuwa makamu wa kapteni, yaani mkuu wa kikosi aliyeshika mamlaka yake wakati hayuko. Maana hiyo ni pia asili ya vyeo vya Luteni Kanali au Luteni Jenerali vilivyotaja manaibu wa kanali au jenerali. Baadaye ziliendelea kuwa vyeo vya pekee bila kuunganishwa na nafasi ya makamu tena. Majeshi ya Afrika yalirithi cheo hicho sawa na vyeo vya kijeshi kwa jumla kutoka mapokeo ...

                                               

Luteni Kanali

Luteni Kanali ni cheo cha afisa wa jeshi, kilicho chini ya Kanali na juu ya Meja. Asili ya neno luteni ni Kifaransa lieu-tenant yaani "mwenye kushika nafasi" kwa maana ya naibu, makamu. Kiasili lieu-tenant alikuwa makamu wa kapteni, yaani mkuu wa kikosi aliyeshika mamlaka yake wakati hayuko. Maana hiyo ni pia asili ya vyeo vya Luteni Kanali au Luteni Jenerali vilivyotaja manaibu wa kanali au jenerali. Baadaye ziliendelea kuwa vyeo vya pekee bila kuunganishwa na nafasi ya makamu tena. Majeshi ya Afrika yalirithi cheo hicho sawa na vyeo vya kijeshi kwa jumla kutoka mapokeo ya jeshi la kikoloni.

                                               

Maharaja

Maharaja ni cheo cha kihistoria kwa mtawala mkabaila nchini Uhindi. Umbo la kike ni maharani ambaye ni ama mke wa maharaja au mtawala wa kike. Cheo hiki kilitumiwa pia katika madola yaliyoathiriwa na Uhindi katika nchi za Indonesia, Malaysia na Ufilipino za leo. Wakati wa utawala wa Kiingereza juu ya Uhindi kulikuwa na madola 600 yaliyokuwa na hali ya nchi lindwa ndani ya Uhindi wa Kiingereza uliojumlisha nchi za Uhindi, Pakistan na Bangladesh za leo. Madola haya yalisimamiwa na watawala ya Kihindi na wengi wao walikuwa na cheo cha maharaja, wengine waliitwa raja, sultani na mengine. Waing ...

                                               

Malkia

Malkia ni mtawala wa kike juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka kwa mzazi wake aliyekuwa mfalme au malkia pia. Lakini kuna pia malkia waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingin,e hasa kama mtawala aliyetangulia alikufa bila mrithi. Mara nyingi malkia alipatikana kwa njia ya ndoa halafu alishika utawala kama mumewe mfalme mwenyewe alikufa au kugonjeka.

                                               

Mtemi

Mtemi ni cheo cha mtawala wa kijadi hasa upande wa bara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye hapo zamani alitawala dola lenye mamlaka kamili katika nchi yenye watu hasa wa jamii moja. Mfano mmojawapo ni Mtemi Mirambo.

                                               

Mwanamke wa Kwanza

Mwanamke wa Kwanza ni cheo kisicho rasmi ambacho hupewa mke wa rais au mkuu wa nchi asiye mfalme au Kaisari. Nchini Marekani, mke wa gavana wa jimbo pia huitwa "Mwanamke wa Kwanza".

                                               

Nahodha

Nahodha ni mtu ambaye anaongoza meli au timu fulani. Kwa kawaida nahodha hutumika katika kitengo cha kijeshi, kwa kamanda wa meli, ndege au chombo kingine, au kamanda wa bandari, idara ya moto au idara ya polisi, idara ya uchaguzi, n.k. Afisa Mkuu anaweza kutumiwa kwa usawa na nahodha katika hali fulani, kama wakati afisa-nany anayehudumu kama kamanda wa meli. Neno la Kiingereza kwa "nahodha" ni "captain" linalotokana na Kigiriki katepánō "aliyewekwa juu" ambalo lilitumiwa kama cheo cha kijeshi. Lilikuwa na asili ya Kilatini kama capetanus / catepan, na maana yake inaonekana kuwa imeungani ...

                                               

Negus

Negus ni cheo cha kifalme katika historia ya Uhabeshi au Ethiopia. Maana ya neno hili ni "mfalme". Cheo hiki kilitumiwa katika historia ya Ethiopia na watawala mbalimbali wa majimbo kwa mfano wa Shewa, Gonder, Tigray na Gojam. Mtawala mkuu wa Ethiopia alitumia cheo cha "Negus Negesti" pia: "Negusa Nagast" au mfalme wa wafalme kinacholingana na "Kaisari". Negus wa mwisho alikuwa tangu 1928 Ras Tafari Makonnen aliyeendela kuwa Kaisari Haile Selassie I tangu 1930. Alipinduliwa na kuuawa na wanajeshi wa Derg waliomaliza utawala wa kifalme katika Ethiopia.

                                               

Omukama

Omukama ni cheo alichopewa kiongozi mkuu wa kabila la Wahaya mkoani Kagera nchini Tanzania. Mfano wake ni Kabaka wa Waganda. Neno hili kwa Kihaya na Kinyambo lina maana ya mkuu au mfalme, na jina la kiongozi huyo aliitwa Lumanyika. Koo-Mtwale, mkuu wa himaya au sehemu iliyo chini ya Mkama. Mtwale anamwakilisha Omkama kwa shughuli za kimila na sheria. Mtwale mara nyingi anaamua kesi ndogondogo kama za ndani ya ndoa, koo, wizi na ugomvi wa majirani na watu. Lakini kuna sehemu kama za eneo la Kiziba ambalo lilikuwa na mfalme wake ambaye alichagua viongozi wa hadhi ya juu, ambao waliitwa Omula ...

                                               

Rais

Rais ni cheo cha mkuu wa nchi katika serikali ya jamhuri, na pengine mkuu wa taasisi fulani. Rais wa nchi huwa anachaguliwa ama na wananchi wote au na bunge. Katika nchi kadhaa kuna pia mkutano maalumu unaoitishwa kwa uchaguzi wa rais pekee, kama vile Marekani au Ujerumani. Kuna aina mbili za rais kufuatana na katiba za nchi mbalimbali: rais kama mkuu wa nchi asiyeshughulikia mambo ya serikali, jinsi ilivyo Ujerumani au Uhindi serikali ya kibunge rais kama mkuu wa serikali, jinsi ilivyo Marekani na pia katika nchi nyingi za Afrika serikali ya kiraisi. Katika muundo wa serikali ya kibunge s ...

                                               

Sayyid

Kimsingi "sayyid" yamaanisha "Bwana": ni namna ya kumtaja mtu kwa heshima. Hutumiwa hivyo katika nchi nyingi za Waarabu. Katika lahaja ya Moroko yafupishwa kuwa "sidi" kutoka sayyidi - Bwana wangu.

                                               

Shah

Shah ni neno la Kiajemi ambalo linamaanisha mfalme au mtawala wa nchi. Neno hilo linatumika katika nchi tofauti ulimwenguni, zikiwa pamoja na Iran, Uhindi, Pakistan na Afghanistan. Hivi sasa neno "Shah" linatumika kama jina la kawaida kwa watu wengi nchini Uhindi, Pakistan na Afghanistan ambao ni Wahindu, Waislamu na Wajaini. Majina mengi ya Kihindi ambayo yana Shah ndani yake; maarufu kati yake ni Shah Jahan, ambaye kama Mfalme wa India aliamuru kuundwa kwa Taj Mahal. Tamko katika mchezo wa sataranji "checkmate" hutokana na Kiajemi shah mat", maana yake "mfalme amekamatwa" Neno "Shah" mar ...

                                               

Spika

Spika ni cheo cha mwenyekiti wa bunge katika nchi zinazofuata urithi wa kisiasa wa Uingereza. Nchi nyingi zilizokuwa koloni za Uingereza kama vile Marekani, Uhindi, Tanzania, Kenya, Nigeria, Australia au New Zealand huwa na cheo hiki hasa zikitumia lugha ya Kiingereza kama lugha rasmi. Neno la Kiingereza limepokelewa pia katika lugha ya Kiswahili. Katika nchi zisizo na urithi wa Kiingereza vyeo kama mwenyekiti au rais wa bunge hutumiwa. Kazi yake ni kuratibu shughuli na majadiliano ya bunge. Huamua juu ya maswali ya utaratibu bungeni, ufuatano wa wabunge katika majadiliano, kutangaza matok ...

                                               

Tenno

Tenno ni cheo cha mfalme au kaisari wa Japani. Kufuatana na katiba ya nchi yeye ni "ishara wa dola na wa umoja wa taifa". Tenno wa sasa ni Naruhito tangu mwaka 2019, alipomrithi baba yake.

                                               

Zumbe

Zumbe ni neno la kisambaa linaloonyesha heshima na uthamani wa mtu, maana yake halisi kwa kisambaa ni Mfalme. Kiongozi wa wasambaa aliitwa Zumbe kama cheo chenye sifa kubwa kwa jamii hiyo. Huko usambaani neno Zumbe pia hutumika kama salamu tangulizi unapogonga kwenye nyumba ya mtu kwa ajili ya kusalimia, yaani lazima utangulize zumbe kwa ajili ya heshima ya baba mwenye nyumba. Katika siku za karibuni huko Usambaani, neno zumbe linatumika kumuonyesha mtu aliye na hali nzuri kimaisha au kimapato. Mfano mtu anapokuwa na hali zuri kimaisha wasambaa kumuita zumbe, yaani wakimaanisha mtu mwenye ...

Cheo
                                               

Cheo

Cheo ni rejeo linaloongezwa kwa jina la mtu kuonyesha heshima, wadhifa au kazi yake. Pia ni kimo cha kitu fulani, kama vile vazi. Tena ni jina la vifaa mbalimbali: mti wa kufulia nazi, ubao mwembamba wa kushonea mkeka, kifimbo cha kuagulia ambacho mganga wa jadi anatafuta vitu.

                                               

Ofisa

Ofisa ni mtu mwenye cheo katika ofisi au katika mfumo wa shirika fulani. Neno latumiwa hasa kwa wanajeshi wa vyeo vyenye mamlaka juu ya wanajeshi wa kawaida. Katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania vyeo vya maofisa vimepokewa kutoka jeshi la kikoloni vikifuata mfumo wa jeshi la Uingereza. Maofisa hutofautishwa baina ya wenye kamisheni ambavyo ni vyeo vya juu zaidi na maafisa wa ngazi za chini.

Admirali
                                               

Admirali

Admerali ni cheo cha kiongozi mkuu wa kijeshi wa wanamaji. Cheo hicho kinalingana na jenerali katika matawi mengine ya jeshi. Neno linatokana na Kiarabu أمير البحر amir-al-bahr yaani "mwenye mamlaka baharini". Iliingia katika lugha za Ulaya kama "admiral". Cheo hicho si kawaida katika jeshi la majini la Tanzania wala Kenya, lakini hutumiwa kutafsiri vyeo vya kigeni.

                                               

Chansela (elimu)

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Chansela ni kiongozi wa chuo kikuu. Matumizi ya cheo hiki katika Kiswahili na lugha nyingine yanatokana na mapokeo ya Uingereza yaliyoenea kupitia makoloni yake na kuendelea katika idadi ya nchi huru. Vinginevyo mkuu wa chuo kikuu mara nyingi huitwa "rais wa chuo". Vyuo vingi katika Jumuiya ya Madola huwa na chansela ambaye si mtendaji mkuu. Katika hali hiyo, mtendaji mkuu huwa ni makamu wake.

                                               

Dame

Dame kwa Kiingereza ni cheo cha chini kwa mkabaila wa kike. Inalingana na cheo cha "Sir". Kwa maana hii hupatikana nchini Uingereza na katika nchi za Jumuiya ya Madola zinazomkubali malkia wa Uingereza kama mkuu wa dola. Siku hizi cheo hiki ama kinarithiwa katika familia zilizokuwa zamani watawala wa makabaila au kinatolewa kwa heshima na kama kitambulisho cha kazi nzuri ya kujitolea katika utumishi wa umma. Kwa Kijerumani neno linapatikana kama namna ya kumsemesha mama kiheshima.

Farao
                                               

Farao

Farao lilikuwa jina la heshima ambalo kila mfalme wa Misri ya kale alipewa. Jina hilo lilitumika hadi Warumi walipoiteka Misri mwaka 30 KK. Farao wa mwisho alikuwa malkia Kleopatra. Kabla ya hapo, wafalme wa kale wa Misri walikuwa na majina matatu: Horus, Nesu Bety na Nebty. Maarufu zaidi ni Ramses II aliyekuwa farao wa masimulizi ya Biblia kuhusu Musa, pamoja na Tutankhamun ambaye ni farao wa pekee ambaye kaburi lake lilihifadhiwa bila kuporwa na majambazi.

Jenerali
                                               

Jenerali

Jenerali ni cheo kikuu cha kijeshi katika nchi nyingi za dunia. Jenerali huwa kiongozi wa ngazi ya juu katika jeshi. Idadi ya majenerali si kubwa. Kazi yao ni kuongoza na kupanga kazi ya jeshi. Kwa kawaida hawashiriki wenyewe katika mapigano. Neno limeingia katika Kiswahili kutoka lugha ya Kiingereza. Asili yake ni Kilatini generalis yenye maana ya "kwa ujumla".

                                               

Kamanda

Kamanda ni cheo cha afisa wa nevi na jeshi la anga kilicho chini ya Nahodha na juu ya Luteni Kamanda. Cheo cha kamanda pia hupatikana katika baadhi ya vikosi vya polisi.

                                               

Kiranja Mkuu

Kiranja Mkuu au Mkuu wa viranja ni kiongozi wa serikali ya wanafunzi shuleni, hasa katika shule ya msingi na sekondari. Kiranja ni mwanafunzi aliyechaguliwa na walimu au wanafunzi wenzake kwa lengo la kuwasimamia usafi, nidhamu, mazingira ya wanafunzi na kuweka daraja kati ya waalimu na wanafunzi. Kiranja Mkuu ndiye anayewasimamia na kuwaagiza viranja wengine, ni kama Rais na wizara zake.

Luteni jenerali
                                               

Luteni jenerali

Luteni jenerali ni ofisa wa jeshi mwenye cheo cha juu kuliko meja jenerali na chini ya jenerali. Luteni jenerali wa jeshi la Tanzania kwa sasa ni Yakubu Hasan.

Luteni wa Pili
                                               

Luteni wa Pili

Luteni wa Pili, pia Luteni-usu, ni cheo cha chini kabisa cha afisa wa jeshi waliopewa kazi ya usimamizi. Kiko chini ya Luteni wa Kwanza.

                                               

Meja Jenerali

Meja Jenerali ni cheo cha afisa wa jeshi kilicho chini ya Luteni Jenerali na juu ya Brigedia au Brigedia Jenerali, kulingana na nchi.

Mwinjilisti
                                               

Mwinjilisti

Mwinjilisti ni Mkristo mwenye utume wa kuhubiri na kutoa elimu ya Biblia na maadili ya Kikristo katika madhehebu kadhaa ya Uprotestanti. Majukumu yake yanafanana na yale ya katekista au ya shemasi wa Kanisa Katoliki.