Back

ⓘ Usafiri
                                               

Usafiri

Usafiri ni uhamisho wa watu au vitu na bidhaa kutoka mahali pamoja kwenda mahali pengine. Usafiri unakuja pamoja na muundombinu kama njia za usafiri, vyombo vya usafiri na wahusika wake kama makampuni, shirika na abiria.

                                               

Chombo cha usafiri

Chombo cha usafiri ni kifaa chochote kinachotumiwa kusafirisha watu au mizigo. Vyombo vya usafiri hutofautiana kama vinahudumia usafiri wa nchi kavu, wa majini au wa hewani. Mifano ni Usafiri wa nchi kati hutumia motokaa, treni, baisikeli au pikipiki Usafiri wa majini hutumia meli, boti, jahazi na mengine Usafiri wa hewani hutumia ndege, helikopta au ndegeputo Hutofautishwa pia kama vinalenga matumizi ya watu binafsi au matumizi ya umma. Baisikeli, pikipiki na motokaa mara nyingi hutumiwa na wenye chombo hiki cha usafiri. Lakini zinaweza kutumiwa pia kama sehemu ya usafiri wa umma kwa mfan ...

                                               

Usafiri nchini Tanzania

Usafiri nchini Tanzania ni hasa kwa njia ya barabara. Nyingine ni reli na ndege. Kwenye maziwa makubwa na pwani ya Bahari Hindi kuna pia usafiri wa meli.

                                               

Usafiri wa anga-nje

Usafiri wa anga-nje ni kila aina za safari au usafiri inayofikia nje za angahewa ya Dunia kwenye anga-nje. Ilhali hakuna mpaka kamili baina ya angahewa na anga-nje kuna mapatano ya kutazama umbali wa kilomita 100 kama chanzo cha anga-nje Chombo cha kwanza kilichofikia juu ya km 100 kilikuwa roketi ya Kijerumani aina ya V-2 katika majaribio ya mwaka 1944. Chanzo cha usafiri wa anga-nje kilikuwa kuruka kwa chombo cha angani cha Kisovyieti Sputnik 1 mnamo 4 Oktoba 1957 iliyokuwa satelaiti ya kwanza iliyozunguka Dunia angani. Kiumbehai wa kwanza aliyefikishwa hadi anga-nje alikuwa mbwa Laika k ...

                                               

Ushirika wa Usafiri wa Hamburg HVV

Ushirika wa Usafiri wa Hamburg ni kampuni ya umma inayoendesha usafiri wa umma katika jiji la Hamburg na maeneo ya karibu katika majimbo ya Niedersachsen na Schleswig-Holstein.

                                               

ESA

ESA ni kifupi cha Kiingereza cha European Space Agency ". Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 1975 na nchi 10 za Umoja wa Ulaya. Wajibu wake ni kuratibu miradi ya nchi za Ulaya ya kuendesha utafiti na uchunguzi wa anga. Shabaha ni hasa kuendeleza juhudi za nchi za Ulaya katika teknolojia ya angani iliyokuwa nyuma sana kulingana na kazi za Marekani na Urusi wakati ule. Mwaka 2014 kulikuwa na nchi wanachama 20, na kati ya hizo kuna nchi 18 wanachama wa Umoja wa Ulaya pamoja na Uswisi na Norwei. Kufuatana na katiba yake, ESA inalenga shabaha zisizo za kijeshi pekee. ESA inashirikiana kwa karibu na ...

                                               

Baisikeli

Baisikeli ni chombo cha usafiri kinachoendeshwa kwa nguvu ya misuli ya binadamu. Baisikeli huwa na magurudumu mawili yanayoshikwa na fremu, kiti kimoja, kanyagio, breki na usukani. Tabia nyingine za kawaida ni kuwa na taa mbele na nyuma. Baisikeli bora huwa pia na gia zinazorahisisha kazi ya kukanyaga kanyagio. Kwa kawaida nguvu hupelekwa kwa nyororo kutoka kanyagio kwenda gurudumu la nyuma. Magurudumu huwa na matairi yaliyojaa hewa. Katika nchi nyingi baisikeli ni chombo muhimu cha usafiri. Zamani baisikeli ilikuwa usafiri wa maskini lakini pia katika nchi kadhaa zilizoendelea watu hutumi ...

                                               

Safari

Safari ni neno la kutaja mwendo au harakati ya watu kutoka mahali fulani kwenda mahali pa mbali angalau kiasi. Safari inaweza kufanywa ama kwa miguu au kwa chombo cha safari au usafiri fulani. Kama safari inazidi muda wa siku mmoja vituo vya safari yaani mahali ambapo msafiri anakaa au analala hadi kuendelea ni sehemu za safari yake. Kuna safari ndefu na safari fupi. Harakati inayotumia muda mfupi tu kama dakika chache au kwa umbali mdogo huitwi safari isipokuwa kwa lugha ya kutaania.

                                               

Reli

Reli ni mfumo wa usafiri wa abiria na mizigo kwa treni zinazotembea juu ya vyuma pau za feleji. Reli ni sehemu muhimu za miundombinu wa nchi. Kwa maana asilia "reli" ni zile "reli za chuma" au reli za garimoshi ambazo kwa kawaida hutumiwa mbili-mbili kijozi kufanya njia ya reli yenyewe. Kwa nchi nyingi reli ni mtindo muhimu wa usafiri kwa sababu inarahisisha mwendo wa watu na bidhaa. Ikitumiwa vema gharama zake ni afadhali kuhusu usafiri wa barabarani. Mahitaji ya nishati kwa kiwango cha mzigo ni kidogo kuliko barabarani. Faida yake ni hasa tabia za njia yake; reli za garimoshi huwa na uso ...

                                               

Pikipiki

Pikipiki ni chombo cha usafiri chenye magurudumu mawili kinachoendeshwa kwa nguvu ya injini ama ya mwako ndani ama ya umeme. Chanzo cha pikipiki kilikuwa baisikeli iliyoongezwa injini.

                                               

Alama ya barabarani

Alama ya barabarani ni alama inayowekwa kwenye nguzo kando ya barabara ili kutoa habari, onyo au elekezo kwa watu wanaopita hapo kwa vyombo vya usafiri au kwa miguu. Alama ya barabarani hutumia picha au matini mafupi ya neno moja au maneno machache kwa madereva au watumiaji wengine wa barabara. Alama hizo huainishwa hivi: alama za maelekezo na taarifa. Alama hizo hutoa maelekezo juu ya utumiaji bora wa barabara au uelekeo, na huwa katika umbo la pembe nne na mara nyingi kwa rangi ya buluu, kijani au nyekundu. alama za michoro ya sakafuni zinazodokeza njia maalum, mahali pa kusimama, nafasi ...

                                               

Alama za kimataifa za magari

Alama za kimataifa za magari ni herufi zinazoonyesha ni nchi gani gari fulani inapotoka. Utaratibu huu ulianzishwa kwa mapatano ya kimataifa kuhusu usafiri kwa magari wa 1926. Ukasahihishwa mara ya mwisho katika mapatano ya kimataifa ya Vienna kuhusu usafiri wa barabarani wa 1968. Orodha lifuatalo hufuata ufuatano wa alama hizi ambao si sawa na ufuatano wa majina ya nchi. Kwa mfano alama za nchi za Kenya, Tanzania na Uganda hazipatikana chini ya herufi K, T au U kwa sababu zote zaanza kwa "EA" kwa "East Africa". Kwa hiyo njia rahisi ya kupata nchi maalumu ni kutumia nafasi ya kutafuta ya k ...

                                               

Barabara ya hariri

Barabara ya hariri ilikuwa njia muhimu ya biashara kati ya China kwa upande mmoja na Afrika Mashariki, Mashariki ya Kati halafu Ulaya kwa upande mwingine. Biashara hiyo iliendelea tangu karne za kabla ya Kristo. Jina la "barabara ya hariri" limetokana na hariri ambayo kwa muda mrefu ilitengenezwa katika China pekee ikawa kati ya bidhaa zilizotafutwa sana duniani kwa bei ya juu. Mnamo Juni 2014, UNESCO imetangaza sehemu Changan-Tianshan ya barabara hiyo kuwa mahali pa Urithi wa Dunia.

                                               

Baraste kuu

Baraste kuu ni aina ya barabara pana yenye pande mbili zinazotenganishwa na kila upande magari hufuata mwelekeo moja tu. Kila upande huwa na vichororo viwili au zaidi. Baraste kuu ni aina ya barabara inayowezesha motokaa mengi kusafiri kwa kasi kubwa. Hakuna mikingamano inayozuia mwendo. Kama barara nyingine inakata au baraste mbili zinakutana kuna madaraja na njia za kando ambako motokaa inaweza kuongeza kasi yake hadi kuingia kati ya magari mengine. Hairuhusiwi kusimama au kupumzika kwenye vichororo vya baraste kuu isipokuwa kwenye nafasi kando ya njia iliyotengwa kwa dharura na maeneo y ...

                                               

Basi

Basi ni chombo cha usafiri kinachotumika kusafirisha watu kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa ajili ya shughuli mbalimbali, kwa mfano kazi, masomo, utafiti na kadhalika. Vyombo hivi vipo vya aina mbalimbali, kwa mfano kuna mabasi madogo yanayobeba abiria wachache na kusafiri umbali wa kawaida, pia kuna mabasi makubwa yenye kubeba watu wengi kuanzia hamsini na kuendelea na mabasi hayo husafiri umbali mrefu: yanaweza kusafiri kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine bila kumpumzishwa. Katika dunia ya sasa mabasi yanatumika sana katika shughuli mbalimbali, kwa mfano shughuli za kiuchumi kwa ...

                                               

Biashara ya misafara

Biashara ya misafara ilikuwa aina ya biashara ambayo ilifanyika kwa kusafirisha bidhaa kwa njia za nchi kavu kwa kutumia wanyama au wapagazi waliobeba mizigo ya msafara. Kwa vipindi virefu vya historia biashara ya misafara ilikuwa njia kuu ya biashara kwenye nchi kavu. Katika maeneo yaliyosimamiwa na serikali fulani wafanyabiashara waliweza kusafiri peke yao, lakini mara nyingi kulikuwa na maeneo au vipindi vya histora ambako usalama njiani ulikosekana. Hivyo wafanyabiashara walilazimishwa kuungana na kusafiri pamoja na kupeana ulinzi au kukodi walinzi. Walitumia ngamia, farasi, punda au w ...

                                               

Boda boda

boda ni neno la kutaja baisikeli inayotumiwa kubeba abiria katika Afrika ya Mashariki au "baisikeli ya teksi". Linaweza kumtaja pia dereva wa baisikeli hii. Asili yake ni kati ya Wajaluo wa eneo la mpakani kati ya Kenya na Uganda karibu na ziwa Viktoria. Inasemekana asili yake ilikuwa huduma ya kubeba abiria kati ya mipaka ya Kenya na Uganda mjini Busia. Hivyo neno la Kiingereza la "border" = "boda" lilikuwa chanzo cha jina "boda-boda" Lakini huduma imeenea sehemu mbalimbali kama vile pwani ya Kenya Mombasa, Malindi na pia katika Uganda. Baisikeli ya kawaida inayotakiwa imara hubadilishwa ...

                                               

Dira

Ndani ya dira ya kawaida kuna sindano ya chuma sumaku inayotazama muda wote kwa ncha ya kaskazini kwa sababu inaathiriwa na uga sumaku wa dunia. Wachina walikuwa watu wa kwanza wanaojulikana kubuni dira wakati wa karne ya 11. Walitumia sindano ya maginetiti iliyoelea kwenye bakuli ya maji juu ya ubao au karatasi. Kuna dira kavu ambako sindano ya sumaku inalala juu ya mhimili. Aina nyingine ambayo ni bora lakini ghali zaidi ni dira kiowevu ambako sindano inaelea ndani ya kiowevu cha mchanganyiko wa alikoholi na maji. Chini ya sindano huwa na kadi yenye mchoro wa mielekeo ya dunia ya kaskazi ...

                                               

Eleveta

Eleveta, pia: lifti, kipandishi, kambarau ni chombo cha kupandisha na kushusha watu au mizigo. Mara nyingi eleveta hutumiwa katika majengo ya ghorofa. Zinatokea pia nje ya majengo kwa mfano katika migodi ambako zinaweza kufika mamia ya mamita chini ya ardhi. Kwa kawaida eleveta ni chumba chenye mlango kinachovutwa kwa kamba au kupandishwa kwa namna ya jeki kati ya ghorofa inapofika. Watu huingia ndani wanapoweza kuchagua ni ghorofa ipi wanapotaka kufika kwa kubofya kitufe ukutani. Milango inafungwa na chumba cha eleveta hupanda au kushuka jinsi inavyotakiwa. Siku hizi eleveta huendeshwa kw ...

                                               

Global Positioning System

Global Positioning System ni mfumo wa kupima na kutambua kwa makini kila mahali duniani ukitumia satelaiti.

                                               

Helikopta

Helikopta ni aina ya chombo cha usafiri wa anga ambacho hakina magurudumu, ila mapanga yazungukayo kwa juu yake. Hayo yanakiwezesha kuinuka na kutua wima mahali popote pakavu, kwenda mbele au kurudi nyuma, kuelea angani na hata kujongea kiupandeupande. Tabia hizo zinaruhusu helikopta kutumika katika maeneo yaliyojaa au yaliyotengwa ambapo ndege haziwezi kufanya kazi kutokana na jinsi ilivyoundwa. Kuna aina mbalimbali za helikopta kama helikopta za uzimaji moto, za vita n.k. Jina helikopta hutoka katika neno la Kiingereza helicopter ambalo limetoholewa kutoka katika neno la Kifaransa helico ...

                                               

Hija

Hija ni ziara ya kidini yaani ni safari inayofanyika kwa sababu ya dini, ikilenga patakatifu fulani. Kwa maana ya kiroho, maisha yote ni safari ya kumuelekea Mungu au uzima wa milele n.k. Sababu ya kwenda mahali maalumu ni tumaini la kuwa karibu zaidi na imani mahali ambako mambo muhimu ya historia ya dini husika yalitokea; mara nyingi pia imani ya kwamba sala itakuwa na nguvu au mafanikio zaidi pale. Desturi ya kuhiji iko katika dini mbalimbali. Waislamu huwa na hajj kutembelea Makka, Washia wanatembela pia makaburi ya maimamu wao huko Najaf, Karbala, Mashhad na penginepo. Mwislamu aliyet ...

                                               

Kitimaguru

Kitimaguru ni kifaa kilichotengenezwa kikiwa na kiti pamoja na magurudumu kwa madhumuni ya kumsaidia majeruhi, wagonjwa wasio na nguvu ya kutembea au watu wenye ulemavu kukalia na kujisukuma, kusukumwa na mtu mwingine au kujiendesha kwa mashine za otomatiki kwa lengo la kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Kiti hicho huwa kimeundwa hivi kwamba mgonjwa atapata starehe ya kuketi. Kitimaguru kinaweza kusukumwa na mtu aliyekikalia au na mwingine anayemhudumia. Huenda pia kikawa na vidhibiti ili anayebebwa aweze kudhibiti mwendo wa kigari kile. Kitimaguru hupatikana pia kwa wenye ulemavu ...

                                               

Kontena

Kontena ni sanduku kubwa la metali -hasa feleji- ambayo vipimo vyake vimesanifishwa kwa matumizi ya kimataifa. Kontena hutumiwa kutunza na kusafirisha bidhaa za kila aina kwa meli, lori au reli. Kontena ndogo husafirishwa pia kwa ndege. Kontena zimepunguza sana kiwango cha kazi na gharama kinachohitajika kusafirisha mizigo. Zilianza kutokea mnamo 1956 huko Marekani kwa matumizi ya mizigo ya kijeshi zikaenea pia upande wa meli za kiraia.

                                               

Mabasi ya mwendokasi

Mabasi ya mwendokasi ni mfumo wa usafiri wa mjini ambako kuna njia za pekee za mabasi kwenye barabara zinazofungwa kwa magari madogo, mabasi ya kawaida na baisikeli. Katika mfumo huu mabasi ya mwendokasi hupewa kipaumbele kwenye njiapanda. Kuna pia mbinu za kuwezesha abiria kuingia na kuondoka pamoja na kukata tiketi haraka. Kwa njia hiyo uwezo wa mabasi ya kubeba abiria wengi huongezwa na kuepukana na matatizo ya mabasi ya mjini ya kawaida ambayo yanaweza kukwama katika msongamano wa magari. Kwa njia hiyo mfumo wa mabasi ya mwendokasi ina faida zinazopatikana vinginevyo kwa mfumo wa metro ...

                                               

Meli za abiria Marekani

Meli ni chombo cha usafiri kiendacho majini. Chombo hicho hutumika hasa katika kusafirisha mizigo mizito kama vile magari na vitu vingine vingi, lakini hata kusafiriha watu. Kwa mfano nchini Marekani meli hutumika kubebea mizigo pia hutumiwa na watu katika safari nchini humo. Meli hizo hujulikana kwa jina la Cruise. Meli hizi huwa kubwa sana, zenye fahari nyingi ndani yake kama vile sehemu za kuogelea, sehemu za michezo,miziki, kula na kulala. Safari zake huwa za muda mrefu kwa sababu huendeshwa kwa mwendo wa kawaida, hivyo safari zake huchukua takriban siku tatu na zaidi kulingana na umba ...

                                               

Mpagazi

Kwa matumizi mengine ya jina Hamali angalia hapa Hamali Mpagazi ni mtu anayembebea mtu mwingine mizigo yake.

                                               

Nauli

Nauli ni ada inayolipwa na abiria kwa matumizi ya chombo cha usafiri wa umma kama vile reli, basi, teksi, ndege n.k. Muundo wa nauli ni mfumo uliowekwa kuamua ni kiasi gani kinachopaswa kulipwa na abiria anuwai wanaotumia usafiri fulani wakati wowote. Nauli inayolipwa ni mchango kwa gharama za uendeshaji wa mfumo wa usafirishaji unaohusika, ama kisehemu jinsi ilivyo kawaida na mifumo inayoungwa mkono na umma au jumla. Katika mifumo mingi ya usafiri abiria hukata tiketi kabla ya kuanza safari inayolipa gharama hadi kufika mwisho wa safari yake. Nauli inaweza kuwa kwa bei moja kwa matumizi y ...

                                               

Njia ya bomba

Njia ya bomba ni mfumo wa kusafirisha vimiminika kama mafuta ya petroli au gesi hadi umbali mkubwa kwa kutumia mabomba yaliyounganishwa. Kuna pia njia za bomba zinazosafirisha madini au makaa yaliyochanganywa na maji kwa kusudi hili. Matumizi mengine ni kwa ajili ya maji safi, maji taka, maziwa au bia.

                                               

Nyumba ya wageni

Nyumba ya wageni ni jengo penye nafasi za kukodi kwa kulala wageni. Ndani yake kuna sehemu ya mapokezi, vyumba vya kulala na nafasi za bafu. Mara nyingi huwa pia na sehemu ya kupata chakula au angalau vinywaji.

                                               

Riksho

Riksho ni chombo cha usafiri ambacho kiasili kilikuwa gari dogo lenye kiti lililovutwa na mtu, ilhali abiria amekalia nyuma.

                                               

Shehena

Shehena inamaanisha mzigo wa bidhaa ambazo zinasafirishwa, mara nyingi kwa kutumia chombo cha usafiri kama vile lori, treni, meli au eropleni. Kihistoria, na hadi leo katika maeneo yasiyo na njia nzuri, shehena zilisafirishwa pia kwa njia ya wapagazi na wanyama kama vile punda, farasi au ngamia. Vyombo vya usafiri wa shehena kwa kawaida hutengenezwa kwa namna ya pekee inayolingana na shehena yake. Tangu kuenea kwa kontena zenye vipimo sanifu, vyombo vya usafiri vya shehena vimesanifishwa pia ili kulingana na vipimo vile, hasa malori, mabehewa ya reli na meli. Shehena hupatikana kwa maumbo ...

                                               

Shirika la ndege

Shirika la ndege ni kampuni inayotoa huduma ya usafiri wa anga wa kiraia kwa abiria na mizigo. Mashirika ya ndege hutumia ndege kutoa huduma hizi. Kawaida, mashirika haya hupewa leseni na idara husika ya serikali. Mashirika ya ndege hutofautiana kwa ukubwa, toka mashirika ya ndege madogo ya safari za ndani na mashirika makubwa ya safari za kimataifa. Mnamo 2019 shirika la ndege kubwa kuliko yote duniani ni American Airlines Group.

                                               

Sleji

Sleji ni kitolori bila magurudumu kinachovutwa na wanyama au watu kikiteleza hasa juu ya theluji au barafu. Ni chombo cha usafiri kikuu kati ya Eskimo wa nchi za aktiki. Ni usafiri wa kawaida pia katika sehemu nyingine baridi penye theluji nyingi. Ni pia chombo cha michezo au burudani pale ambako theluji inapatikana kwa muda fulani tu. Kuna pia aina za sleji zinazotumiwa pasipo na theluji lakini kwa kawaida magari yenye magurudumu yalichukua nafasi zao.

                                               

Treni ya umeme

Treni ya umeme ni tofauti na treni nyingine zinazotumia mafuta ili kuweza kutembea.Treni ya umeme hutumia nishati ya umeme kutembea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa haraka sana, tofauti na treni za mafuta. Treni hizi za umeme hubeba abiria tu na kwenda kwa mwendo kasi wa zaidi ya kilomita mia tatu kwa saa moja. Pia kuna kiyoyozi kizuri kwa ajili ya kuweka baridi ndani ya treni kwani madirisha ya treni hii huwa hayafunguki. Ndani mna huduma mbalimbali kama vile huduma za chakula na vinywaji, huduma ya mapumziko yaani kulala, hata huduma ya mtandao. Huduma hii ya mtandao huwawez ...

                                               

Chuo Kikuu cha Kifaransa cha Elimu ya Usafiri Angani

Chuo Kikuu cha Kifaransa cha Elimu ya Usafiri Angani ni chuo kikuu cha Ufaransa kinachofundisha fani zote za usafiri wa angani kama vile urubani, uhandisi wa eropleni au usimamizi wa mwendo wa eropleni hewani. Chuo hiki kilianzishwa mwaka 1949 mjini Orly karibu na Paris lakini tangu 1968 kilihamishwa kwenda Toulouse ambako kuna pia viwanda vikubwa vya eropleni hasa vya Airbus na kampuni ya usafiri wa anga-nje EADS.

Abiria
                                               

Abiria

Abiria ni watu wanaosafiri kwa kupanda meli, ndege, gari, basi, pikipiki au treni. Abiria hutumia vyombo hivyo vya usafiri kama njia ni mbali, au kama hawana usafiri wa binafsi au kama wanapendelea matumizi ya usafiri wa umma kuliko usafiri wao binafsi. Kwa kawaida wakipanda wanalipia kiasi fulani kama nauli ili mwenye chombo hicho aweze kuwalipa dereva na wahudumu wengine pamoja na gharama za chombo chenyewe na matumizi yake.

                                               

Ndege

Ndege ni neno ambalo kwa Kiswahili linaweza kumaanisha: Ndege mnyama ni aina wa wanyama ambao kwa kawaida wanaweza kuruka. Ndege uanahewa au eropleni ni chombo cha usafiri kinachoweza kuruka wakati kikiwa na abiria au mizigo ndani yake.

                                               

Barabara ya mchipuko

Barabara ya mchipuko ni njia ambayo hutumika pale ambapo kunakuwa na matengenezo ya barabara ambapo mchipuko husaidia kupunguza msongamano wa magari hasa katika miji mikubwa. Barabara hizi husaidia pia kurahisisha usafirishaji wa mizigo pamoja na abiria kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.