Back

ⓘ Sayansi ya Jamii
                                               

Sayansi ya Jamii

Sayansi ya jamii ni somo kuhusu jamii za binadamu. Ni sayansi ya kijamii ambayo hutumia mbinu mbalimbali za uchunguzi kwa kupima ili kutengeneza na kusafisha mwili wa maarifa na nadharia kuhusu shughuli za kijamii za binadamu. Mara nyingi huwa na lengo la kuyatumia maarifa hayo ili kuisaidia jamii. Mada mbalimbali katika sayansi ya kijamii ni kama vile eneo dogo la kiwakala na mwingiliano hadi eneo kubwa la mifumo na miundo ya kijamii. Sayansi ya jamii ni taaluma pana sana ukitazama mbinu inayotumia na mada inazolenga. Taaluma zake za kijadi zimekuwa ni mpango wa jamii yaani, uhusiano wa w ...

                                               

Sayansi

Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa. Mara nyingi Galileo Galilei anahesabiwa kuwa baba wa sayansi ya kisasa.

                                               

Émile Durkheim

Émile Durkheim alikuwa mtaalamu kutoka Ufaransa aliyeweka misingi ya sosholojia au sayansi ya jamii. Aliunda mbinu za kuchunguza muundo wa jamii.

                                               

Sosholojia

Sosholojia ni fani ya sayansi inayochunguza mwenendo wa kijamii, yaani binadamu katika maisha ya jamii: unavyoanza, unayoendelea, unavyojipanga na unavyosababisha miundo. Kwa maneno mengine, sosholojia inamsoma mtu katika mahusiano yake: mtu na mtu, mtu na watu kundi na hivyo huweza kugundua tabia zake mbalimbali. Somo hilo linahusiana na masomo mengine, kama vile anthropolojia, historia, saikolojia na uchumi. Ni mojawapo kati ya sayansi za jamii nayo inatumia mbinu tofauti za kutambua hali halisi, halafu inazichunguza kimpango.

                                               

Usanifu majengo

Usanifu majengo ni sanaa na sayansi ya kubuni muundo na sura ya majengo. Sanaa na sayansi hii inajumuisha pia mambo kama mipango miji, usanifu wa eneo la kujenga, na hata ubunifu wa samani zitakazotumika ndani ya jengo. Watu wanaojihusisha na haya huitwa "wasanifu majengo". Wanahitaji elimu ya ujenzi, hesabu, sanaa, teknolojia, elimu jamii na historia. Msanifu wa kwanza anayejulikana kwa jina ni Imhotep wa Misri ya Kale. Mbinu za usanifu hutegemea teknolojia inayopatikana, hali ya hewa, hali ya jamii, utaratibu wa siasa yake, hali ya uchumi na mengine mengine. Nchi na tamaduni mbalimbali z ...

                                               

Jumba la Makumbusho

Jumba la Makumbusho ni jengo au taasisi penye maonyesho ya vitu vya kale, kazi za sanaa, sampuli za malighafi au vifaa kwa ajili ya kutunza kumbukumbu ya jamii. Mkusanyiko wa aina hii hulenga kuonyesha mifano ya sanaa, utamaduni, teknolojia au mazingira asilia kwa manufaa ya kuwaelimisha watazamaji. Kuna majumba ya makumbusho ya aina mbalimbali yanayokazia fani fulani za elimu kama vile makumbusho ya historia, ya sanaa, ya teknolojia ya sayansi na kadhalika. Kati ya majumba ya makumbusho mashuhuri duniani ni Makumbusho ya Vatikani mjini Roma makumbusho ya Britania mjini London Louvre mjini ...

                                               

Umma

Umma ni jumla ya watu wote katika kikundi, jamii au nchi. Kisosholojia, umma ni watu walio na nia sawa katika jambo fulani kama vile, wasomaji wa gazeti, watazamaji wa televisheni au kandanda ama watumiaji wa mtandao. Katika sayansi ya siasa, umma ni wananchi wakilinganishwa na serikali ambayo hudhaniwa kuwa mtu. Serikali humiliki mali ya umma kwa niaba ya wananchi wake. Vilevile, huduma zozote zinazotolewa na serikali husemekana kuwa za umma kwa sababu umma wananchi ndio huigharamia serikali kwa wafanyakazi, kodi, ushuru, n.k. Kwa mfano, shule za umma.

                                               

Kiingereza

Kiingereza ni lugha ya jamii ya Kigermanik cha Magharibi iliyokua nchini Uingereza kwa muda wa miaka 1.400. Leo, zaidi ya wasemaji milioni mia nne duniani wanazumgumza Kiingereza kama lugha ya kwanza. Watu wengi zaidi wanazumgumza Kiingereza kama lugha ya pili, kwa sababu ni muhimu sana kwenye nyanja za mawasiliano, sayansi na uchumi wa kimataifa.

                                               

Maendeleo

Kwa matumizi tofauti ya jina hili angalia hapa Maendeleo Maendeleo ni mabadiliko yanayoonekana kuboresha hali ya binadamu. Hali hiyo inajitokeza katika nyanja mbalimbali za maisha na kulisha mawazo mengi. Upande wa sayansi yanahusika na ongezeko la ujuzi kutokana na utafiti na mabadilishano ya matokeo yake. Upande wa historia yanahusishwa na utambuzi wa kwamba ulimwengu unaweza kuboreshwa zaidi na zaidi kutokana na mchango wa sayansi, teknolojia, uhuru n.k. Upande wa jamii yanahusishwa na tarajio la kwamba binadamu anaweza kupata hali bora zaidi na zaidi katika mafungamano, siasa, uchumi n ...

                                               

Teknolojia

Teknolojia: "uwezo, usanii, ufundi". Teknolojia inaweza kumaanisha: uwezo wa kubadili malighafi asilia na kuwa bidhaa yenye thamani inayoweza kukidhi mahitaji ya binadamu. Hapa bidhaa haimaanishi tu vitu kama magodoro, magari ya kutembelea, unga wa ngano n.k., la hasha: ni huduma yoyote inayotolewa kwa jamii, mfano huduma ya usafiri, huduma ya utalii, huduma ya chakula, na pamoja na vitu vyote vinavyozalishwa viwandani. elimu ya matumizi yake pamoja na mbinu na maarifa jinsi ya kutumia sayansi vifaa na mashine zinazotumika katika matengenezo au uzalishaji wa vitu Teknolojia nyepesi kabisa ...

Demografia
                                               

Demografia

Demografia ni sayansi ya jamii inayozingatia takwimu za idadi ya binadamu. Inaweza kuhusu mabadiliko yoyote ya makundi ya watu mbalimbali kadiri ya mahali na wakati, k. mf. kulingana na wengine kuzaliwa, kufa, kuhama, kuzeeka na kufa.

                                               

Fani

Kwa matumizi tofauti ya neno hili angalia makala Fani Fani kutoka ar. فنع "bora" ni uwanja maalumu wa elimu, maarifa au kazi. Kutaja kazi fulani kuwa "fani" kunahitaji kiwango fulani wa ubora au taaluma. Mifano ya fani katika ufundi ni pamoja na useremala, ujenzi, uhunzi, upishi au uchoraji. Mifano ya fani katika sayansi au elimu ya juu ni pamoja na sayansi jamii kama vile historia, ualimu, falsafa, isimu, fasihi, sosholojia sayansi asilia kama vile fizikia, kemia, astronomia, biolojia, tiba

Mipango miji
                                               

Mipango miji

Mipango miji ni sayansi na sera kuhusu maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kimazingira katika miji na vitongoji vyake. Mgiriki Hippodamus anasemekana kuwa ndiye baba wa mipango miji kutokana na ubunifu wake wa mji wa Miletus ingawa kumekuwa na miji iliyopangwa kabla yake. Taaluma ya mipango miji imechipuka toka kwenye taaluma za usanifu majengo na uhandisi.

Users also searched:

maswali na majibu darasa la saba, maswali ya uraia na maadili darasa la nne,

...
...
...