Back

ⓘ Mashirika
                                               

Mashirika ya ombaomba

Watawa wa kike hawakuweza kufuata mtindo uleule: waliishi kimonaki lakini kwa kuzingatia ufukara na udugu wa Kifransisko na kwa kuombea utume wa hao ndugu wadogo. Klara wa Asizi 1193-1253," mche mdogo” wa Fransisko, ndiye mwanamke wa kwanza kutunga kanuni ya kitawa. Tapo hilo ni maarufu kwa marekebisho yaliyofuatana hadi leo kuhusu ufukara. Tangu karne XII wanawake wengine pia walichangia sana ustawi wa utawa, wa maisha ya Kiroho na wa Kanisa kwa jumla hata kwa maandishi yao. Kati yao Katerina wa Siena 1347-1380, wa utawa wa tatu wa Mt. Dominiko, ametangazwa kuwa mwalimu wa Kanisa.

                                               

Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga

Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga ni umoja wa kimataifa wa kampuni za usafiri kwa ndege. Makao makuu yake yako Montreal, Quebec nchini Kanada ambako kuna pia makao makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa Kiraia. IATA ilianzishwa mwaka 1945 ili kujenga ushirikiano wa makampuni makubwa ya ndege. Leo hii kuna takriban kampuni wanachama 240. Haya ni hasa makampuni ya kitaifa au makampuni makubwa ya kibiashara yanayotoa huduma za kimataifa. Mashirika madogo yanayohudumia nchi moja tu, pamoja na mashirika ya ndege za kukodi, mara nyingi si wanachama. Kati ya kazi za IATA ni jitihada za kusa ...

                                               

Mashirika ya kilimwengu

Mashirika ya kilimwengu ni mashirika yaliyokubaliwa na viongozi wa Kanisa Katoliki kwa waamini wanaojisikia wito wa kushika mashauri ya Kiinjili kama watawa, lakini si lazima kwa kuishi kijumuia.

                                               

Mtawa

Mtawa ni mtu anayejitenga na ulimwengu ili kuishi maisha maadilifu. Katika dini mbalimbali, mfano mmojawapo wa utawa ni ule wa wamonaki. Lakini katika Ukristo, hasa wa Magharibi historia ya Utawa ilitokeza aina nyingine mbalimbali. Katika Kanisa Katoliki, ni mwamini yeyote aliyejiweka wakfu kwa Mungu hasa kwa kushika useja mtakatifu, lakini kwa kawaida pia ufukara na utiifu. Mara nyingi watawa wanaunda mashirika yenye karama moja inayofafanuliwa na kuratibiwa katika kanuni na katiba maalumu. Mtawa anaweza kuwa mwanamume au mwanamke, mwenye daraja takatifu au la.

                                               

Historia ya Utawa

Hatuwezi kuelewa utawa tukidhani ni kitu kimoja: jina hilo linajumlisha maisha tofautitofauti. Katika makala hii tunataka kufuata historia ya maisha haya katika Ukristo kama kitabu bora kilichoandikwa na Mungu siku kwa siku kadiri ya mpango wake wa hekima kwa ujenzi wa Kanisa lake takatifu kwa karama za kumshuhudia Yesu katika sifa na kazi zake mbalimbali. Kuna hatua kuu nne zilipozaliwa aina mpya za utawa hasa magharibi bila ya kufuta zile zilizotangulia: 3. Kuanzia karne XVI yalitokea mashirika mengi ya kikleri, yasiyo na nadhiri na ya kutolea huduma maalumu. 1. Kuanzia karne III hadi XI ...

                                               

Ukanoni

Ili kuboresha maisha ya mapadri wanajimbo, toka zamani ulisisitizwa uundaji wa jumuia kati yao, ambamo wasali na kufanya utume kwa pamoja. Hasa kuanzia karne XI wengi walifanya hivyo kwenye makanisa makubwa kama mtindo mpya wa kitawa unaosisitiza liturujia ya fahari pamoja na uchungaji. Inavyoweza kueleweka, hao walifuata kanuni ya Agostino wa Hippo na kuitwa Wakanoni. Maarufu zaidi katika yao ni Norbert 1082-1134, mwanzilishi wa Wapremontree. Leo mtindo huo unaendelea katika mashirika mbalimbali, ambayo lakini hayana watu wengi kama aina nyingine za utawa.

                                               

Majimbo ya Cote dIvoire

Majimbo ya Cote dIvoire ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi nchini. Majimbo yaliundwa mwaka 2011 lakini katika hali nyingi hayajaanza kufanya kazi kama mashirika ya serikali. Kuna majimbo 14, ikiwa ni pamoja na majimbo huru mbili ambazo ni miji ya Yamoussoukro na Abidjan. Ingawa hayajagawanywa katika mikoa, majimbo huru huwa na wilaya kwa Kifaransa: départements, tarafa kwa Kifaransa: sous-prefectures na miji. Majimbo 12 yaliyobaki yamegawanywa katika mikoa 31, ambayo imegawanywa katika wilaya zaidi ya 108. Wilaya hizo zimegawanywa katika tarafa 509.

                                               

Asasi

Asasi ni chombo kikubwa kama vile shirika linalohusika na utoaji wa huduma kwa watu katika jamii. Asasi zipo za aina mbalimbali; kuna asasi za kiserikali na asasi zisizo za kiserikali.

                                               

Wabenedikto

Shirika la Mtakatifu Benedikto, ni utawa wa wamonaki wanaofuata Kanuni ya Mtakatifu Benedikto iliyoandikwa mwaka 534 na kuenea kote Ulaya Magharibi kama namna ya kawaida ya umonaki.

                                               

Habari

Habari ni mawasiliano ya maarifa kuhusu matukio ambayo huwasilishwa kwa watu kwa maneno ya kinywa, kwa maandishi kama vile magazeti, kwa matangazo ya masafa marefu kama vile redio au runinga, kwa intaneti n.k. Neno hili linaweza kutumiwa pia katika sayansi kwa mawasiliano ya habari kwa Kiingereza information, si news kati ya seli za mwili, kwa mfano kati ya mkono na ubongo, kwa njia ya neva.

                                               

Door of Hope Tanzania

Door of Hope to Women and Youth Tanzania ni asasi isiyokuwa ya kiserikali iliyopo katika kata ya Shangani, manispaa ya Mtwara, Tanzania. Ni shirika linaloshugulika kuwainua kina mama na vijana kiakili, kisaikolojia na kimwili ili waweze kufanikiwa na kuwa na maendeleo endelevu.

                                               

Dropping Knowledge

Dropping Knowlege ni shirika lisilo la kiserikali lenye lengo la kuleta majadiliano dunia nzima kuhusu matatizo makubwa yanayomkabili mwanadamu. Tarehe 9 Septemba 2006 shirika hili liliandaa tukio linaloitwa "Meza ya Sauti Huru" the Table of Free Voices, ambapo watu 112 toka katika nyanja mbalimbali kama za sayansi, teknolojia, utamaduni, na sanaa hukaa pamoja na kujibu maswali 100. Maswali haya huchujwa toka katika maswali ambayo huulizwa na watu mbalimbali duniani kupitia tovuti ya shirika hili. Majibu ya maswali haya hurekodiwa na kuandikwa na kuhifadhiwa ili kwa msingi wa baraza liitwa ...

                                               

International Youth Fellowship

IYF ni shirika la lisilokuwa la kiserikali ambalo asili yake ni nchi ya Korea Kusini. Shirika hili linajihusisha na mambo ya vijana katika kubadilisha mawazo na mitazamo ya kimaisha ikijikita kubadilisha akili za vijana katika kupambanua mambo. Shirika hili limekua na kuenea katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Kenya, Tanzania, China, Korea, Malaysia, Ghana, Togo, Rwanda, Australia, USA, Mexico, Peru, Paraguay na nyingine nyingi ambazo hujumuisha vijana katika kubadilishana mawazo juu ya elimu za kijamii na kidini. Kujenga na kuboresha kizazi kijacho *Kujenga viongozi wa baabae kubadili ...

                                               

Life Support For Change

Life Support for Change ni asasi isiyo ya kiserikali wala kifaida iliyoanzishwa na Miriam Oscar Kaaya mwaka 2014 katika kata ya Mbuguni mkoani Arusha ikishughulika na masuala ya watoto na wanawake.

                                               

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai. Makao makuu yako Den Haag. Ni tofauti na Mahakama Kuu ya Kimataifa inayoamua ugomvi kati ya nchi kama pande zote zinakubali kupeleka kesi huko.

                                               

Shirika Lisilo la Kiserikali

Shirika Lisilo la Kiserikali ni maungano ya watu wanaoshirikiana pamoja kwa kulenga shughuli za jamii kwa jumla. Haipokei maagizo kutoka kwa serikali wala hailengi faida ya kifedha kwa watu wanaoendesha shirika. Mashirika yasiyo ya Kiserikali yako kwenye ngazi ya miji, maeneo, kitaifa na kimataifa. Kati ya shirika zisizo za serikali zinazojulikana zaidi kimataifa ni Msalaba Mwekundu, makanisa na vyama vyao kama vile Caritas au Diakonia, shirikia nyingine za kidini zinazotoa huduma za umma, Amnesty International, Madaktari wasio na Mipaka-MSF, Oxfam na wengi wengine. Jumla la shirika zisizo ...

                                               

Ubuntu Hub

Ubuntu Hub ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mkoani Arusha kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo wanaopatikana katika mkoa huo. Asasi hiyo ilianzishwa na Collins Kimaro pamoja na wenzake wawili ambao ni Carolin Kandusi na Jonathan Ruta. Ubuntu wamekuwa wakiandaa mafunzo mbalimbali na elimu kwa ajili ya kuwaelimisha wafanyabiashara na wajasiriamali wanaochipukia katika mbinu bora za kukuza na kupata mawazo ya biashara pamoja na kuwaendeleza katika sekta ya ubunifu.

                                               

Voice Of Youth Tanzania

Voice Of Youth Tanzania ni taasisi inayoshughulika na masuala ya vijana, wanawake na watoto. Ilianzishwa mwaka 2012 na Vincent Uhega na kupata usajili mwaka 2017 / Voice of Youth Tanzania ni asasi isiyokuwa ya kiserikali na ambayo haijiendeshi kifaida yenye makao yake makuu mkoani Arusha katika mji mdogo wa Usa River ndani ya wilaya ya Arumeru. Ni taasisi iliyoanza mara baada ya kumalizika kwa kampeni ya kusaka vipaji kwa vijana wa mtaani iliyojulikana kama Talanta Mtaani

                                               

Zaina Foundation

Zaina Foundation ni asasi isiyo ya kiserikali na ya kifaida iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria mwaka 2017 ikiwalenga sana wanawake na watoto wa kike katika kuwawezesha juu ya matumizi sahihi ya mitandao na mifumo ya kidijitali Taasisi hii imekuwa ikiandaa mafunzo na semina mbalimbali kwa wanawake na watoto wa kike juu ya namna ya kutumia ulinzi katika mitandao ili kujikinga na unyanyasaji wa kijinsia na ulinzi wa kimtandao.

                                               

Mimutie Women Organization

Mimutie Women Organization ni asasi isiyo ya Kiserikali iliyoanzishwa na Rose Njilo kwa ajili ya kuwasaidia na kuwainua wanawake wa jamii ya kifugaji ya Kimaasai katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha. Ni shirikia ambalo linafanya kazi ya kuwainua wanawake hasa Wamaasai likiamini kuwa mwanamke akiinuka kiuchumi atakua na kujijengea heshima.

Shirika la Hali ya Hewa ya Dunia
                                               

Shirika la Hali ya Hewa ya Dunia

Shirika la Hali ya Hewa ya Dunia ni asasi ya ushirikiano baina ya serikali mbalimbali duniani ikiwa na idadi ya Nchi wanachama 193. Makao makuu ya shirika ni Geneva, Uswisi. Rais wa mkutano wa Dunia wa hali ya hewa ndiye kiongozi mkuu wa shirika ambaye ni Gerhard Adrian, na mtangulizi wake alikuwa David Grimes. Shirika hili lilianzishwa baada ya lile la Shirika la Kimataifa la Hali ya Hewa, lililoanzishwa mnamo mwaka 1873.

                                               

United African Alliance Community Center

United African Alliance Community Center ni shirika lisilo la kiserikali lililopo mkoani Arusha. Shirika hilo lilianzishwa mwaka 1991 na Pete ONeal pamoja na mke wake Charlotte Hill ONeal kwa malengo ya kuwasaidia watoto pamoja kuendeleza utamaduni. Shirika hilo linapatikana katika wilaya ya Arumeru, nje kidogo ya mji mdogo wa Usa River na wanafunzi ndani ya kituo hiki hujifunza sanaa, kompyuta, ufundi pamoja na lugha ya Kiingereza na elimu hizo hutolewa bila ya malipo

                                               

Vision For Youth

Vision For Youth ni asasi isiyo ya kiserikali yenye makao yake mkoani Arusha, asasi hii hufanya kazi katika maeneo matatu makuu ambayo ni afya,elimu ya uraia,pamoja na kuwainua vijana kiuchumi. V4Y hufanya kazi kwa vijana wenye umri kuanzia miaka kumi tano hadi thelethini na tano.