Back

ⓘ Afya
                                               

Afya

Afya ni hali ya kujisikia vizuri kimwili, kiakili, kiroho na kiutu bila kusumbuliwa na ugonjwa wowote. Afya ya binadamu itakuwa njema kama atafuatilia kanuni na taratibu bora za afya. Hiyo inajumuisha mlo kamili, yaani chakula chenye virutubishi vyote, vikiwemo protini, wanga na mafuta hiyo iwe katika asilimia ndogo sana. Pia anatakiwa awe msafi mwilini na mazingira yake, kama vile kwa kuoga na kusafisha mazingira yanayomzunguka. Mandhari yenye hewa safi pia husaidia katika kuhifadhi afya ya binadamu katika mwili na akili. Mazingira mara nyingi huchukuliwa kuwa jambo muhimu katika hali ya ...

                                               

Afya ya msingi

Afya ya msingi ni mbinu mpya ya huduma za afya baada ya mkutano wa kimataifa katika Alma Ata mwaka wa 1978 ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani na UNICEF. Afya ya msingi ilikubaliwa na nchi wanachama wa WHO kama hatua muhimu kufikia lengo la Afya kwa wote. Kwa vile watu duniani kote wanakufa moyo zaidi na zaidi katika utowajibikaji wa mifumo ya afya ya leo na huduma za kukidhi mahitaji yao, wito wa mfumo mpya wa afya ya msingi - na afya kwa wote - unaongezeka.

                                               

Afya ya jamii

Afya ya jamii ni kigezo katika afya ya umma ambayo inajihusisha na afya na ubora wa jamii. Wakati jina jamii linaweza kufafanuliwa wazi, afya ya jamii huelekea kuzingatia maeneo ya kijiografia kuliko binadamu wenye sifa sawa. Baadhi ya miradi, kama vile InfoShare au GEOPROJ huchanganya mfumo wa habari za jiografia na mifumo ya habari zilizopo, ili kuruhusu umma kuchunguza tabia ya jamii yoyote katika Marekani. Kwa sababu afya III husukumwa na safu pana ya demografia, vipengele mbalimbali huanza kutoka uwiano wa wakazi wa kundi lenye umri maalum katika matarajio ya kuishi. Hatua za matibabu ...

                                               

Shirika la Afya Duniani

Shirika la Afya Duniani ni kitengo cha Umoja wa Mataifa. Inashughulika habari za afya ya umma ikilenga kuunganisha juhudi za kitaifa za kupambana na magonjwa na kujenga afya. Kisheria WHO ni shirika lenye madola wanachama 193. Kati ya shughuli muhimu za WHO ni progframu za kupambana na magonjwa yanayoathiri watu wengi kama vile Malaria, Ukimwi au SARS. WHO inaratibu mipango ya kutengeneza na kusambaza madawa ya kinga. Inaratibu pia miradi ya chanjo za kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali. Makao makuu ya WHO yapo Geneva Uswisi. Kuna ofisi sita za kikanda kama zifuatazo: Kopenhagen kanda la Ul ...

                                               

Orodha ya kimataifa ya magonjwa na matatizo ya afya

Orodha ya kimataifa ya magonjwa na matatizo ya afya ni orodha ya magonjwa yaliyopangwa katika utaratibu kufuatana namba zao. Ni utaratibu unaokubaliwa kote duniani kwa kutaja na kurekodi magonjwa. Orodha hii inatolewa na Shirika la Afya Duniani. Kulikuwa na matoleo mbalimbali na toleo la kisasa ni ICD-10, toleo la 2006. Toleo jipya la ICD-11 inepangwa kwa mwaka 2015., ambayo itakuwa inapitiwa kwa kutumia Web 2.0. Hii orodha inatumiwa na madaktari, serikali na makampuni ya bima kutaja magonjwa, kukusanya takwimu za sababu za vifo na kupanga shughuli za tiba. Asili ya orodha hii ni kazi ya d ...

                                               

Siri ya Mtungi

Siri ya Mtungi ni tamthilia ya televisheni kutoka nchini Tanzania. Imetayarishwa na Media for Development International MFDI, waliopewa jukumu na Programu ya mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins JHUCCP Tanzania kwa msaada wa watu wa Marekani kupitia USAID. Ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012, imekuwa tamasha maarufu zaidi la televisheni nchini Tanzania na nchi nyingine zinazozungumza Kiswahili. Tamthilia hiyo inawaleta pamoja wasanii bora wa Tanzania, waandishi, wanamitindo wa nguo, wakurugenzi wa sanaa, waigizaji na watendaji wa filamu kwenye mafanikio makubwa ya ukuaj ...

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
                                               

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii) ni wizara ya serikali nchini Tanzania. Ofisi kuu ya wizara hii zipo mjini Dar es Salaam.

Kanuni
                                               

Kanuni

Kanuni ni taratibu zilizotungwa na binadamu ambazo ni lazima kutimizwa. Taratibu hizi zinaweza kuwa za afya, uchumi, biashara, kilimo, dini n.k. Mfano wa kanuni za afya: Osha tunda kwa maji safi kabla ya kulila. Nawa mikono kila baada ya kutoka chooni. Nawa mikono kabla au baada ya kula kwa maji safi na salama.

                                               

Kituo cha afya cha Itololo

Kituo cha Afya Itololo kipo katika wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma na kina namba ya usajili 101996. Kituo hiki cha Itololo kipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa. Kituo cha Itololo ni kituo cha Mishionari cha wamishenari mabradha na mapadre wa Passionist

Barakoa
                                               

Barakoa

Kuna barakoa za kiutamaduni na barakoa za kinga. Mfano mmoja wa barakoa za kiutamaduni ni Barakoa ya Sirige ya Wadogon wa Mali. Pia ni nguo ya wanawake wa Kiislamu ambayo wanaivaa kwenye mapaji ya nyuso zao pamoja na buibui, ijulikanayo kama "burqa". Barakoa za kinga zinavaliwa kwa shughuli mbalimbali, zikilenga kuzuia au kupunguza athira hatari za vumbi, gesi, hewa chafu au viini vya ugonjwa. Tangu kutokea kwa ugonjwa wa corona matumizi yake yameongezeka sana katika nchi nyingi za Dunia.

Chandarua
                                               

Chandarua

Chandarua ni kitambaa cha wavu kinachotundikwa hasa kitandani ili kumkinga mtu asiumwe na mbu anapolala. Pia kinaweza kutundikwa katika madirisha na milango ili wadudu wasiingie ndani. Kwa mbinu hizo binadamu anajaribu kujihami na maradhi yanayosambazwa na mbu na wadudu wengine, kama vile malaria n.k. Siku hizi wengine wanakitia chandarua dawa ya maji ambayo inaweza kuua wadudu wanapokigusa.

Kichefuchefu
                                               

Kichefuchefu

Kichefuchefu ni msukosuko wa moyo unaomfanya mtu kuhisi kinyaa au uchafukaji wa tumbo na baada ya hapo mara nyingi hutapika. Ni dalili mojawapo ya ugonjwa mbalimbali.

Kifungo
                                               

Kifungo

Kifungo ni itifaki ya kisheria inayohusu kuzuia watu wasitoke eneo la gereza. Inaweza kutumika pia kuhusu taarifa.

Kipodozi
                                               

Kipodozi

Kipodozi ni kifaa chochote cha kukwatua ngozi ili kuongeza uzuri wa mtu, hasa mwanamke. Mifano ya vipodozi ni: poda, wanja, losheni, marashi n.k. Baadhi yake vimechanganikana na sumu au kemikali zenye madhara, hivyo vinakatazwa na sheria. Katika nchi za Marekani, kuna sheria ambazo zimekataza kuuza kwa vipodozi ambavyo huenda zikaathiri ngozi ya mtumiaji. Sheria hizi ni kama Federal Food, Drug and Cosmetic Act na Fair Packaging and Labelling Act.

Kula
                                               

Kula

Kula ni kitendo cha kiumbe hai kuingiza chakula ndani ya mwili wake kupitia mdomo wake. Kula humfanya kiumbe hai kuwa na nguvu. Viumbe hai wanahitaji kula ili miili yao iendelee kufanya kazi. Matatizo mbalimbali ya kiafya yanaweza kutokea kiumbe asipopata mlo kamili.

Kunyanyua vyuma
                                               

Kunyanyua vyuma

Kunyanyua vyuma ni moja ya mazoezi maarufu kwa ajili ya kujenga nguvu na kukuza mifupa. Mazoezi ya aina hii hufanywa kwa kunyanyua vyuma vyenye uzito wa aina mbalimbali. Michezo mbalimbali duniani hutumia aina hii ya mazoezi kuimarisha nguvu na afya za wachezaji. Michezo hii ni kama vile mpira wa kikapu, mpira wa miguu, mpira wa magongo, riadha, mieleka, n.k. Pia ni mchezo mmojawapo ambao toka zamani unafanyika katika Olimpiki.