Back

ⓘ Kisiwa cha Pasaka
Kisiwa cha Pasaka
                                     

ⓘ Kisiwa cha Pasaka

Kisiwa cha Pasaka ni kisiwa cha Chile katika Pasifiki ya mashariki takriban 3.526 km kutoka mwambao wa Chile.

Anwani ya kijiografia ni 27°09′S 109°25′W.

Mji mkuu ni Hanga Roa.

Kuna wakazi 5.761 2012.

                                     

1. Jiografia

Kisiwa kiko peke yake baharini: kisiwa cha karibu ni Pitcairn km 2.000 upande wa magharibi.

Kina asili ya kivolkeno. Ni mlima ulioanza kukua chini ya bahari kwenye mgongo mashariki wa Pasifiki mita 3000 chini ya UB.

Umbo la kisiwa ni pembetatu lenye urefu mkubwa wa km 24 na upana mkubwa wa k, 13. Eneo lote ni 162.5 km². Mlima mkubwa hufikia kimo cha 509 m juu ya UB.

Kando ya kisiwa kikuu kuna visiwa vidogo kadhaa bila watu.

                                     

2. Historia

Inaaminika ya kwamba kisiwa kilikaliwa na watu kutoka Austronesia katika milenia ya 1 BK. Walileta nao ndizi, taro, viazi na miwa pamoja na kuku na panya.

Utamaduni wao ulistawi kwa karne kadhaa na alama zake ni sanamu kubwa za vichwa vya mawe kote kisiwani. Vichwa hivi huitwa "Moai" lakini hakuna uhakika kusudi lao lilikuwa nini.

Kuna pia mabaki ya mwandiko uliokuwa mwandiko wa pekee kati ya visiwa vyote vya Polynesia. Inaaminiwa ya kwamba wakati fulani idadi ya wakazi ilifikia 10.000 hadi 15.000.

Lakini utamaduni huo uliporomoka kabla ya kufika kwa Wazungu wa kwanza. Wataalamu huamini ya kwamba wenyeji walipata matatizo ya kiekolojia kwa sababu miti yote ilikatwa na rutuba ya ardhi ilipotea. Wengine huamini ya kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yalikuwa na athira pia.

Wakati wa kufika kwa Waholanzi, waliokuwa Wazungu wa kwanza kukuta kisiwa kile baharini, walibaki watu 2.000 - 3.0000 pekee. Kufika huku kulitokea tarehe 5 Aprili 1722 ambayo ilikuwa siku ya Pasaka: hivyo hilo likawa jina la kisiwa.

Idadi ya wenyeji ikaendelea kushuka kutokana na magonjwa ya nje yaliyokuja na meli zilizopiga hodi kisiwani kila baada ya miaka kadhaa.

Katika karne ya 19 watu mamia walikamatwa na wafanyabiashara ya utumwa.

Chile ilitwaa kisiwa na kukitangaza sehemu ya eneo lake mwaka 1888. Wakati ule kilikuwa na watu 178 pekee. Idadi hii ilikua tena.

Leo hii takriban theluthi mbili ya wakazi ni Rapanui au wenyeji asilia ya kisiwa. Kwa jumla kuna Warapanui 4.647 mwaka 2002: nusu yao wanaishi kisiwani na nusu nyingine Chile bara.

Users also searched:

...
...
...