Back

ⓘ Teinainano
Teinainano
                                     

ⓘ Teinainano

Teinainano ni mji mkuu wa nchi ya visiwani ya Kiribati katika Pasifiki.

Manisipaa ya Teinainano Urban Council - TUC yenye wakazi 36.717 inajumlisha vijiji na miji midogo ya kisiwa kirefu kwenye kusini ya atolli ya Tarawa. Anwani ya kijiografia ni 1°19N 172°58E.

Majengo ya serikali yapo hasa mjini Bairiki ambao ni kisiwa kidogo kilichounganishwa na sehemu nyingine za Teinainano kwa madaraja.

Kuna Chuo cha Ualimu cha Kiribati pamoja na tawi la Chuo Kikuu cha Pasifiki ya Kusini. Kuna pia ofisi kuu za makanaisa makubwa.

Users also searched:

...