Back

ⓘ Visiwa vya Mariana ya Kaskazini
Visiwa vya Mariana ya Kaskazini
                                     

ⓘ Visiwa vya Mariana ya Kaskazini

Visiwa 16 vyenye eneo la kilometa mraba 463 jumla ni sehemu ya funguvisiwa ya Mariana na vikubwa ni Saipan, Tinian na Rota. Sehemu ya kusini ya funguvisiwa ni Guam ambayo pia ni eneo la ngambo la Marekani.

                                     

1. Historia

Wakazi wa kwanza wanaojulikana ni Wachamoru.

Tangu mwaka 1667 visiwa vilikuwa koloni la Hispania.

Baada ya vita ya Marekani dhidi Hispania sehemu ya kusini ya Mariana ikatwaliwa na Marekani. Kaskazini ikauzwa kwa Ujerumani.

Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia makoloni ya Ujerumani ziligawiwa kwa nchi mbalimbali na Mariana ya Kaskazini ziliwekwa chini ya utawala wa Japani.

Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia visiwa vikawa sehemu ya eneo lindwa la Pasifiki lililotawaliwa na Marekani.

Mwaka 1978 visiwa vikapata madaraka ya kujitawala kwa ushirikiano na Marekani. Guam, ambapo kuna kituo muhimu cha kijeshi, inaendelea kuwa kama koloni la Marekani.

                                     

2. Watu

Idadi ya wakazi imefikia 53.883 2010: kati yao 50% wana asili ya Asia. Wakazi asili ni 37.9% tu.

Upande wa dini, wengi wao ni Wakatoliki 64.1%.

Users also searched:

...
...
...