Back

ⓘ Samoa ya Marekani
Samoa ya Marekani
                                     

ⓘ Samoa ya Marekani

Samoa ya Marekani kwa Kisamoa: Amerika Samoa au Samoa Amelika ni Eneo la ngambo la Marekani katika bahari ya Pasifiki upande wa kusini wa nchi huru ya Samoa.

Kuna wakazi 54.719 wengi wakiwa wametokana na wakazi asili katika eneo la nchi kavu la km² 199.

Eneo lake ni sehemu ya funguvisiwa la Samoa. Kutokea kwa eneo la pekee kulisababishwa na ukoloni wa karne ya 19 ambako Ujerumani na Marekani zilishindana juu ya visiwa hivyo. Funguvisiwa liligawiwa kwa mkataba wa Berlin wa 1899. Sehemu ya mashariki ikawa upande wa Marekani na sehemu ya magharibi upande wa Ujerumani.

Kwa katiba ya mwaka 1967 Samoa ya Marekani ilipewa madaraka ya kujitawala.

Upande wa dini, karibu wote ni Wakristo, hasa Wakalvini 50% na Wakatoliki 20%, kama si Wamormoni.

Users also searched:

...
...
...