Back

ⓘ Visiwa vya Cook
Visiwa vya Cook
                                     

ⓘ Visiwa vya Cook

Visiwa vya Cook kwa Kiingereza: Cook Islands, kwa Kimaori: Kūki Āirani ni nchi huru ya Polynesia katika Pasifiki iliyopo katika hali ya ushirikiano wa hiari na Nyuzilandi.

Eneo lake ni visiwa vidogo 15 vyenye eneo la km² 240.

Mji mkuu wa Avarua uko kwenye kisiwa cha Rarotonga.

                                     

1. Historia

Jina limetolewa kwa kumbukumbu ya mpelelezi Mwingereza James Cook aliyefika kwenye kisiwa cha Manuae mwaka 1773 na kuchora visiwa hivi mara ya kwanza kwenye ramani ya dunia.

Visiwa vilikuwa eneo lindwa la Uingereza katika karne ya 19 kufuatana na ombi la malkia wa Cook aliyeogopa uvamizi wa Ufaransa wakati ule.

Chini ya utawala wa Kiingereza viliwekwa chini ya usimamizi wa serikali ya New Zealand, zikabaki hivyo katika hatua mbalimbali za uhuru wa New Zealand.

Mwaka 1965 New Zealand ikawapa watu wa Cook nafasi ya kujiamulia kuhusu uhuru wao. Visiwa viliamua kujitawala katika ushirikiano na New Zealand. Hatua hiyo ilisimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa azimio lake No. 1514 XV.

Sheria huamuliwa na bunge la visiwa vya Cook. Serikali haisimamiwi na New Zealand. Wananchi wote wana uraia wa New Zealand inayoendesha pia shughuli za jeshi na siasa ya nje kwa niaba ya visiwa. Visiwa vya Cook vimebaki na nafasi ya kufanya mapatano na nchi za nje vilevile.

                                     

2. Watu

Wakazi ni 17.379 2016, karibu wote wenye asili ya Kimaori 81.3% na machotara wa Kimaori 6.7%.

Lugha zinazotumika ni hasa Kiingereza 86.4% na Kimaori 76.2%.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo Waprotestanti.

                                     

3. Viungo vya nje

  • Cook Islands Government
  • Cook Islands Biodiversity Database
  • Open Directory Project - Cook Islands directory category
  • Cook Islands - Detailed and non-commercial website
  • Cook Islands, the best kept secret in the Pacific Ocean - The Most Comprehensive Website
  • Cook Islands National Environment Service Archived Oktoba 15, 2008 at the Wayback Machine.
  • Cook Islands Tourism Corporation
  • Cook Islands Government summary

Users also searched:

...
...
...