Back

ⓘ Polynesia ya Kifaransa
Polynesia ya Kifaransa
                                     

ⓘ Polynesia ya Kifaransa

Polynesia ya Kifaransa kwa Kifaransa: Polynésie française ; kwa Kitahiti: Pōrīnetia Farāni ni eneo la ngambo la Ufaransa katika Pasifiki ya kusini. Eneo lake ni mafunguvisiwa mbalimbali ya Polynesia.

Kisiwa kinachojulikana zaidi ni Tahiti pamoja na mji mkuu wake wa Papeete ambayo ni pia mji mkuu wa eneo lote.

                                     

1. Jiografia

Visiwa, funguvisiwa na atolli za Polynesia ya Kifaransa kwa jumla vina eneo la nchi kavu la km² 4.167 jumla vilivyosambazwa katika kilomita za mraba 2.500.000 za bahari.

Visiwa vyote vimegawiwa katika tarafa tano ambazo ni vikundi vya visiwa vyenye mafunguvisiwa ndani yake; ni kama zifuatazo:

  • Visiwa vya Tuamoto-Gambier ni eneo kubwa la Polynesia ya Kifaransa lenye mafunguvisiwa mawili: Tuamoto atolli 76 na Gambier visiwa 26
  • Visiwa vya Marquesas katika kaskazini, karibu zaidi na Hawaii, penye makundi mbili ya visiwa, vya kaskazini na ya kusini
  • Visiwa vya Shirika Visiwa vya Society 13 vyenye asili ya kivolkeno ambavyo ni sehemu yenye wakazi wengi; vimegawiwa katika tarafa mbili za
  • tarafa ya Visiwa upande wa upepo pamoja na kisiwa kikuu cha Tahiti chenye nusu ya wakazi wote wa Polynesia ya Kifaransa
  • tarafa ya Visiwa mbali na upepo
  • Visiwa vya Austral Visiwa vya Kusini vyenye mafunguvisiwa mawili: Tubuaï na Bass.
                                     

2. Watu

Wakazi ni 268.270 sensa ya mwaka 2012, ambao kati yao 2/3 ni Wapolinesia asilia na 11.9% ni Wazungu.

Kati yao wote, 68.5% wanatumia kwa kawaida lugha ya Kifaransa, iliyo lugha rasmi pekee.

Upande wa dini, 54% ni Waprotestanti, 30% ni Wakatoliki, halafu kuna Wamormoni na Mashahidi wa Yehova.

Users also searched:

...
...
...