Back

ⓘ Kaledonia Mpya
Kaledonia Mpya
                                     

ⓘ Kaledonia Mpya

Kaledonia Mpya kwa Kifaransa: Nouvelle-Calédonie - nuvel kaledoni ni eneo la ngambo la Ufaransa katika bahari ya Pasifiki.

Kisiwa kikubwa cha Grande Terre pamoja na visiwa vingine ni sehemu ya Melanesia.

Jumla ya eneo la visiwa vyote ni km² 18.575.

Wakazi ni 268.767 sensa ya mwaka 2014. Kati yao, 39.1% ni Wakanaki, ambao ni wa jamii ya Wamelanesia na ndio wakazi asili wa visiwa hivyo. Walau 30% ni Wazungu, wengine wana asili ya Polinesia na Asia Kusini Mashariki.

Kifaransa ndiyo lugha inayotumika zaidi.

Upande wa dini, karibu wote ni Wakristo: 50% ni Wakatoliki, wengine Waprotestanti.

Mji mkuu ni Nouméa.

Hadi sasa pesa ni Franc ya pasifiki lakini kuna majadiliano kutumia Euro jinsi ilivyo kwa Ufaransa bara.

Watu wa Kaledonia Mpya wamepiga kura tarehe 4 Novemba 2018 na 56.40% wamependelea kuendelea kuwa sehemu ya Ufaransa, si kujitegemea kama nchi huru.

                                     

1. Viungo vya nje

  • Government of New Caledonia Kifaransa
  • New Caledonia: picture post card beautiful Archived Aprili 16, 2013 at the Wayback Machine. - Official Government of France website in English
  • Tourism New Caledonia
  • Kaledonia Mpya katika Open Directory Project
  • Biodiversité Néo-Calédonienne

Users also searched:

...
...
...