Back

ⓘ Tuvalu
Tuvalu
                                     

ⓘ Tuvalu

Tuvalu ni nchi ya visiwani ya Polynesia katika Bahari ya Pasifiki kati ya Hawaii na Australia. Nchi jirani katika bahari ni Kiribati, Samoa na Fiji.

Jina la Tuvalu lamaanisha "visiwa vinane" kwa sababu kiasili kulikuwa na visiwa 8 tu vilivyokaliwa na watu. Kisiwa cha tisa kimepata wakazi tangu mwaka 1943.

                                     

1. Eneo

Eneo lake ni visiwa vinne na atolli tano; kwa jumla eneo lina 26 km².

Kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa Tuvalu ni nchi yenye wakazi wachache kabisa.

Tuvalu ina visiwa na atolli vifuatavyo:

 • Niulakita
 • Nukufetau
 • Nanumea
 • Nanumaga
 • Nukulaelae
 • Vaitupu
 • Funafuti
 • Nui
 • Niutao
                                     

2. Nchi itakayopotea karibuni

Kama nchi mbalimbali za visiwani Tuvalu iko katika hatari ya kupotea katika miaka 50 inayokuja. Kimo cha juu cha visiwa vyake ni mita 5 pekee juu ya UB. Kubadilika kwa hali ya hewa duniani na kupanda kwa uwiano wa bahari kutamaanisha ya kwamba sehemu kubwa sana la eneo lake litazama polepole chini ya maji.

Serikali imeshaomba majirani wakubwa kama Australia na New Zealand kuwapokea wenyeji wake.

New Zealand imekubali na kwa sasa kila mwaka watu 75 wanahamia New Zealand ambayo ni tayari kuwapokea pia wengine itakapokuwa lazima. Kuna mipango ya kuwapa makazi ya pamoja kwa kusaidia kuhifadhi utamaduni wao.

                                     

3. Historia

Tuvalu imekaliwa na watu wa Polynesia tangu zamani miaka 3.000 hivi iliyopita.

Iliwekwa chini ya usimamizi wa Uingereza katika karne ya 19 kwa jina la "Ellis Islands".

Kati ya 1892 hadi 1916 ilikuwa eneo lindwa na baadaye sehemu ya koloni la Gilbert and Ellice Islands hadi 1974.

Mwaka ule wenyeji walipigia kura pendekezo la kuwa pekee, mbali na visiwa vya Gilbert vilivyokuwa Kiribati baadaye. Tuvalu ikapata uhuru wake mwaka 1978.

                                     

4. Lugha na dini

Kuna lugha tatu tu ambazo huzungumzwa nchini Tuvalu, yaani Kiingereza, Kituvalu na Kikiribati.

Upande wa dini, karibu wakazi wote ni Waprotestanti 97%.

                                     

5. Viungo vya Nje

 • Open Directory Project - Tuvalu Archived Mei 9, 2008 at the Wayback Machine. directory category
 • Effects of Climate Change on Tuvalu
 • Official Website of the Government of Tuvalu Archived Septemba 16, 2007 at the Wayback Machine.
 • Story on Global Warming Effects on Tuvalu
 • PBS Rough Cut: Tuvalu: That Sinking Feeling
 • TuvaluIslands.com
 • Timeless Tuvalu - The Official Travel Website of Tuvalu

Users also searched:

...
...
...