Back

ⓘ Nauru
Nauru
                                     

ⓘ Nauru

Nauru ni nchi ya kisiwani ya Mikronesia katika Pasifiki ya kusini.

Ni nchi ndogo sana ya tatu baada ya Vatikani na Monaco, yenye km² 21 pekee na wakazi wasiofikia 10.000.

Kisiwa jirani zaidi ni Banaba katika Kiribati chenye umbali wa km 300.

Nauru haina mji mkuu rasmi.

                                     

1. Historia

Nauru imekaliwa na mchanganyiko wa watu kutoka Polynesia na Mikronesia tangu karne nyingi miaka 3.000 hivi.

Katika karne ya 19 kisiwa kilitwaliwa na Ujerumani kama sehemu ya makoloni yake ya Pasifiki.

Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia kilikuwa eneo lindwa chini ya Umoja wa Mataifa UM na utawala ulikuwa mikononi mwa nchi tatu: Australia, New Zealand na Uingereza.

Uhuru ulipatikana tangu 1968.

                                     

2. Watu

Wakazi wengi 58% ni wenyeji, wakifuatwa na watu kutoka visiwa vingine vya Pasifiki 26%, Wazungu 8% na Wachina 8%.

Karibu wote 95% ni wanene mno, hivyo hali ya afya si nzuri, hasa upande wa kisukari 40%.

Lugha

Kuna lugha tatu tu ambazo huzungumzwa nchini Nauru: Kiingereza lugha rasmi, Kinauru lugha ya mawasiliano, na pijini inayounganisha Kiingereza, Kichina na Kiaustronesia.

Dini

Wakazi wengi ni Wakristo Waprotestanti na Wakatoliki kwa uwiano wa 2:1, wakifuatwa na wafuasi wa Bahai 10% na Wabuddha 9%.

                                     

3. Uchumi

Uchumi wa Nauru ulitegemea fosfeti iliyopatikana kisiwani kwa wingi. Kwa miaka kadhaa kisiwa kilikuwa nchi tajiri kabisa. Hadi mwaka 2001 huduma za hospitali zilikuwa bure, hapakuwa na kodi, na watu wengi walikuwa na magari mawili au matatu.

Tangu kumalizika kwa fosfeti hali ya kiuchumi imekuwa ngumu sana. 90% za wananchi wanakosa kazi. Serikali haina pesa za kutosha tena, huduma nyingi zimekwama, hata imeanza kupokea misaada kutoka Australia.

Users also searched:

...
...
...