Back

ⓘ Tonga
Tonga
                                     

ⓘ Tonga

Tonga ni nchi ya visiwani ya Polynesia katika Pasifiki ya kusini yenye wakazi 102.321.

Eneo lake ni funguvisiwa lenye visiwa 169 kusini kwa Fiji na Samoa na kaskazini kwa New Zealand. Visiwa 52 tu vina wakazi.

                                     

1. Jiografia

Eneo lote la nchi kavu ya visiwa ni km² 750.

Kisiwa kikubwa ni Tongatapu chenye eneo la km² 260.

Mahali pa juu katika Tonga ni volkeno ya mlima wa Kao ambacho ni kisiwa cha Kao chenyewe wenye kimo cha mita 1.030.

                                     

2. Lugha na dini

Kuna lugha tatu tu ambazo huzungumzwa nchini Tonga: Kiingereza lugha rasmi, Kitonga lugha rasmi na Kiniuafo’ou ambayo imeanza kufifia.

Upande wa dini, 90% wanajitambulisha kama Wakristo, hasa Wamethodisti 38% na Wakatoliki 15%, mbali ya Wamormoni 18%.

Users also searched:

...
...
...