Back

ⓘ Samoa
Samoa
                                     

ⓘ Samoa

Samoa ni nchi ya visiwani ya Polynesia katika Pasifiki ya kusini yenye wakazi 176.710 2001 sensa. Nchi huru ya Samoa ni sehemu ya magharibi ya funguvisiwa ya Samoa. Sehemu ya mashariki iko chini ya Marekani.

                                     

1. Jiografia

Eneo lake ni visiwa tisa au kumi kama kisiwa kidogo sana kinahesabiwa humo, jumla ni kilomita za mraba 2.934. Visiwa viwili vikubwa vya Upolu km² 1.118 na Savaii km² 1.708 vina asilimia 96 za eneo lote. Kuna bado visiwa viwili vidogo vya Manono na Apolima vyenye wakazi, halafu visiwa vingine visivyokaliwa na watu.

Mji mkuu wa Apia uko Upolu.

Mahali pa juu ni mlima Mauga Silisili mwenye kimo cha mita 1.858.

                                     

2. Historia

Samoa ilikaliwa na Waaustronesia tangu miaka 3.000 iliyopita.

Mzungu wa kwanza alifika mwaka 1722.

Ilikuwa ufalme wa kujitegemea kabisa hadi mwaka 1889. Mwaka ule uliwekwa chini ya ulinzi wa nchi tatu: Uingereza, Ujerumani na Marekani.

Baada ya kifo cha mfalme 1898 kulitokea fitina juu ya mrithi wake na nchi za nje zilingia kati. Mkataba wa Pande Tatu wa mwaka 1899 uligawa funguvisiwa ya Samoa kati ya Ujerumani na Marekani. Sehemu ya magharibi ikawa "Samoa ya Kijerumani".

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia visiwa vilitekwa na New Zealand vikabaki chini ya nchi hiyo kama maeneo yaliyokabidhiwa na Shirikisho la Mataifa na baada ya 1945 na Umoja wa Mataifa kwa jina la "Samoa ya Magharibi".

Uhuru ulipatikana mwaka 1962.

                                     

3. Lugha na Dini

Wakazi ni 194.320, karibu wote wakiwa wametokana na wakazi asili.

Kuna lugha mbili tu ambazo huzungumzwa nchini Samoa, zote mbili zikiwa lugha rasmi, yaani Kiingereza na Kisamoa.

Upande wa dini, karibu wote ni Wakristo, wengi wakiwa Waprotestanti, hasa Wakalvini 31.8%, wakifuatwa na Wakatoliki 19.4%.

Users also searched:

...
...
...