Back

ⓘ Palau
Palau
                                     

ⓘ Palau

Palau kwa Kipalau: Belau ni nchi ya visiwani ya Mikronesia katika Bahari ya Pasifiki. Iko takriban km 500 upande wa mashariki wa Ufilipino.

Jumla kuna visiwa 250 hadi 350: idadi inategemea namna gani mtazamaji anapendelea kuhesabu sehemu ya nchi kavu kuwa kisiwa kufuatana na ukubwa au udogo wake. Visiwa tisa vimekaliwa na watu na kisiwa kikubwa chenye km² 331 ni Babelthuap.

Hadi mwaka 1994 ilikuwa nchi lindwa chini ya Marekani kwa niaba ya Umoja wa Mataifa. Marekani inaendelea kuwajibika kwa mambo ya kijeshi kufuatana na mkataba uliofanywa baada ya uhuru.

Mji mkuu ni Melekeok kwenye kisiwa cha Babelthuap.

Wakazi ni 18.000 hivi, ambao 70% ni wenyeji wenye asili mchanganyiko kutoka visiwa vya Pasifiki.

Kuna lugha tano ambazo huzungumzwa nchini Palau.

Upande wa dini, 49.5% ni Wakatoliki, 21.3% Waprotestanti mbali ya 5.3% ambao ni Waadventista Wasabato. 8.7% wanafuata dini ya Modekngei ambayo inachanganya Ukristo na dini ya jadi.

Users also searched:

gharama za passport tanzania, immigration tanzania passport tracking, www passport application form online,

...
...
...