Back

ⓘ Visiwa vya Solomon
Visiwa vya Solomon
                                     

ⓘ Visiwa vya Solomon

Visiwa vya Solomon ni nchi ya visiwani ya Melanesia katika Bahari ya Pasifiki iliyoko mashariki kwa Papua Guinea Mpya.

Eneo lake ni visiwa karibu 1000, vyenye jumla ya km² 28.400 na wakazi 652.857, wengi wakiwa Wamelanesia 95.3%, wakiongea lugha 90. Lugha rasmi ni Kiingereza.

Kati yao 97.4% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Anglikana na Katoliki 19%.

Mji mkuu ni Honiara kwenye kisiwa cha Guadalcanal.

                                     

1. Historia

Visiwa vimekaliwa tangu miaka elfu kadhaa na Wamelanesia.

Kuanzia karne ya 19 vilikuwa koloni la Ujerumani na la Uingereza.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mapigano makali kati ya Japani na Marekani yalitokea hapo.

Visiwa vilipata uhuru mwaka 1978.

Users also searched:

...
...
...