Back

ⓘ Melanesia
Melanesia
                                     

ⓘ Melanesia

Melanesia ni eneo la Bahari ya Pasifiki lililoko kaskazini kwa Australia. Ni mojawapo kati ya makundi makubwa matatu ya visiwa vya Pasifiki pamoja na Mikronesia na Polynesia.

Jina lake limeundwa na maneno ya Kigiriki μέλας cheusi na νῆσος kisiwa yaani "visiwa vyeusi" au zaidi "Visiwa vya Weusi". Nahodha Mfaransa Jules Dumont dUrville alitunga jina hilo mwaka 1832 akitaka kutaja wazawa waliokuwa na rangi nyeusi-nyeusi.

                                     

1. Watu na utamaduni

DUrville alijumlisha wakazi wa visiwa hivyo pamoja kutokana na rangi yao. Lakini hali halisi ni watu wa aina mbalimbali. Wengine ni Waaustronesia, wengine Wapapua na wengine wametokana na mchanganyiko wa vikundi hivyo viwili.

                                     

2. Nchi za Melanesia

Fiji, Papua Guinea Mpya, Visiwa vya Solomon, Vanuatu na Kaledonia Mpya chini ya Ufaransa zinajihesabu kuwa sehemu za Melanesia. Kuhusu visiwa vingine mawazo hutofautiana.

                                     

3. Visiwa vya Melanesia

Visiwa na mafunguvisiwa vifuatavyo vinahesabiwa katika Melanesia:

 • Visiwa vya Torres Strait
 • Palau
 • Visiwa vya Maluku
 • Fiji
 • Vanuatu
 • Guinea Mpya Papua Guinea Mpya pamoja na jimbo la Papua la Indonesia.
 • Kaledonia Mpya
 • Funguvisiwa la Bismarck
 • Visiwa vya Solomon

Visiwa vilivyoko katika eneo hili lakini wakazi hawajitazami kuwa Wamelanesia:

 • Timor
 • Nauru
 • Flores
 • Sumba

Wakati mwingine hata visiwa upande wa Guinea Mpya vinahesabiwa humo ingawa wakazi hawajitazami hivyo: Halmahera, Alor na Pantar.

Users also searched:

...
...
...