Back

ⓘ Vanuatu
Vanuatu
                                     

ⓘ Vanuatu

Vanuatu ni nchi ya visiwani ya Melanesia katika Bahari ya Pasifiki ya kusini yenye visiwa 83.

Iko takriban km 1.750 mashariki kwa Australia, km 500 kaskazini-mashariki kwa Kaledonia Mpya, magharibi kwa Fiji na kusini kwa Visiwa vya Solomon.

Mji mkuu ni Port Vila.

                                     

1. Watu

Kuna wakazi 266.937 2014 wakiongea lugha asili 113 angalia orodha ya lugha za Vanuatu.

Lugha rasmi ni Bislama, Kiingereza Kifaransa.

Wakazi wana asili ya Melanesia. Inawezekana watu wa kwanza walihamia visiwani miaka 4.000 iliyopita.

Kwa sasa wengi ni Wakristo, hasa Waprotestanti Wakalvini, Waanglikana n.k., halafu Wakatoliki 15%.

Users also searched:

...
...
...