Back

ⓘ Dado
Dado
                                     

ⓘ Dado

Dado alikuwa askofu na waziri wa Wafaranki.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Agosti.

                                     

1. Maisha

Mtoto wa mtakatifu Authaire Audecharius, alilelewa katika ikulu ya mfalme Chlothar II aliyefariki 629, ambapo alipata elimu na uanajeshi pamoja na vijana wengine wa koo maarufu.

Baadaye alisimamia mali ya Dagobert I, akishika sana maadili na akiwa na marafiki kama watakatifu Wandregisel, Didier wa Cahors na Eligius, ambaye Ouen aliandika habari za maisha yake.

Mwaka 635 pamoja na ndugu zake Ado na Rado alianzisha abasia ya Rebais, halafu monasteri ya Mt. Wandrille huko Rouen, na nyingine ya kike huko Fécamp. Fredegar reports that even as court referendary, Audoin had a reputation of being a religious man.

Mwaka 641 alifanywa askofu wa Rouen.