Back

ⓘ Waamori
Waamori
                                     

ⓘ Waamori

Waamori walikuwa watu wa jamii ya Wasemiti kutoka Syria walioenea pia katika maeneo makubwa ya Mesopotamia kusini kuanzia karne ya 21 KK hadi mwisho wa karne ya 17 KK, wakianzisha idadi kadhaa ya miji-dola muhimu, hasa Babuloni.

Kisha kufukuzwa kutoka Mesopotamia, huko Syria walitawaliwa kwanza na Wahiti, halafu na Waashuru tangu 1365.

Baada ya 1200 KK hawaonekani tena: inaonekana walimezwa na Wasemiti wengine, ambao kati yao walijitokea hasa Waaramu.

                                     

1. Katika Biblia

Katika Biblia Waamori ni wakazi wa milima ya Kaanani, ambao kadiri ya kitabu cha Mwanzo 10:16 wametokana na Kanaan, mwana wa Hamu na mjukuu wa Nuhu. Wanaonekana kama sehemu ya Wakaanani.

Wanatajwa kama watu warefu sana kama "mierezi" Am 2:9. Mfalme wao Ogu anatajwa kama jitu la mwisho Kumb 3:11.

                                     

2. Marejeo

  • E. Chiera, Sumerian Epics and Myths, Chicago, 1934, Nos.58 and 112;
  • E. Chiera, Sumerian Texts of Varied Contents, Chicago, 1934, No.3.;
  • H. Frankfort, AAO, pp. 54–8;
  • F.R. Fraus, FWH, I 1954;
  • G. Roux, Ancient Iraq, London, 1980.

Users also searched:

...
...
...