Back

ⓘ Kutubu
Kutubu
                                     

ⓘ Kutubu

Kutubu ni nyota angavu zaidi katika kundinyota la Dubu Mdogo. Nyota hii iko karibu sana na nukta ya ncha ya kaskazini ya angani na kabla ya kupatikana kwa teknolojia ya kisasa ilikuwa nyota muhimu kwa ajili ya mabaharia waliotazama angakaskazi. Haionekani kwenye nusutufe ya kusini ya Dunia.

                                     

1. Jina

Kutubu ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini upande wa kaskazini wa ikweta wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema القطب al-qutub inayomaanisha "nyota ya ncha ya kaskazini".

Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulikubali jina la Kilatini na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Polaris".

Alfa Ursae Minoris ni jina la Bayer ikiwa ni nyota angavu zaidi katika Dubu Mdogo na Alfa ni herufi ya kwanza katika Alfabeti ya Kigiriki.

                                     

2. Tabia

Kutubu iko kwa umbali wa miaka nuru takriban 323 - 433 kutoka Jua letu, tofauti ya namba inatokana na vipimo vinavyoofautiana hadi sasa bila kupata usuluhisho. Mwangaza unaoonekana ni mag 1.98.

Kutubu ni nyota maradufu yenye sehemu tatu: nyota kuu inayojulikana kama α Umi Aa au A 1 inayozungukwa na msindikaji mdogo α Umi Ab au A 2 na hizi mbili zinazungukana na nyota ya tatu α Umi B kitovu cha graviti cha pamoja.

Kutubu ilitambuliwa kwenye mwaka 1780 na William Herschel kwa darubini kuwa nyota maradufu yaani mfumo wa nyota mbili za α Umi na α Umi B. Wakati ule darubini ya Herschel ilikuwa kati ya vifaa bora duniani. Kwa kutumia Darubini ya Angani ya Hubble ilitambuliwa kwenye mwaka 2006 ya kwamba pia nyota ya A yenyewe ni nyota maradufu na sasa Polaris yote inajulikana kama mfumo wa nyota tatu zinazoitwa α Umi A 1, α Umi A 2 na α Umi B.

Nyota kuu ni Kutubu A 1 Polaris Aa ambayo ni nyota badilifu yenye masi ya Jua mara 5 iking’mara 1200 kuliko Jua letu. Kutokana na mng’aro mkubwa inapangwa katika kundi la nyota jitu kuu. Mwangaza wa α Umi Aa ulibadilikabadilika kati ya mag 1.86 hadi 2.13 wakati wa kurekodiwa kama miaka 100 iliyopita. Baadaye kiwango hiki kilipungua kwa muda mrefu lakini kwa miaka ya nyuma kimeanza kuongezeka tena

                                     

3. Kutubu kama Nyota ya Ncha ya Kaskazini

Mtazamaji kwenye nusutufe ya kazkazini ya Dunia anaona nyota ya Kutubu inakaa mahali pake ilhali nyota zote zingine zinazunguka wakati wa usiku. Hali halisi inazunguka pia kidogo lakini haitambuliki na mtazamaji maana haiko kikamilifu kwenye ncha ya anga bali kwa umbali wa nyuzi 0.7°.

Katika kumbukumbu za kale si Kutubu iliyoangaliwa kuwa nyota ya kuonyesha mwelekeo wa kaskazini. Ptolemaio aliitaja kama "kwenye mkia wa Dubu Mdogo" Miaka 2000 iliyopita nyota iliyokuwa karibu zaidi na ncha ya kaskazini ya anga ilikuwa Kochab β Ursae Minoris. Kutokana na kusogea kwa mhimili wa mzunguko ing. en:precession pia Kutubu imefika katika nafasi hii takriban miaka 400 iliyopita na bado inaendelea kukaribia hadi mwaka 2100; baadaye itaendelea polepole kusogea tena mbali na ncha ya kaskazini ya anga. Baada ya miaka 12.000, nyota ya Vega katika Kinubi itakuwa nyota ya ncha ya kaskazini jinsi ilivyowahi kuwa miaka 14.000 iliyopita.

                                     

4. Viungo vya Nje

 • Constellation Guide:Ursa Minor
 • Ursa Minor, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, Star Tales, iliangaliwa Oktoba 2017
 • Polaris Alfa Ursae Minoris, kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
                                     

5. Marejeo

 • Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
 • Lee, B. C.; Mkrtichian, D. E.; Han, I.; Park, M. G.; Kim, K. M. 2008. "Precise Radial Velocities of Polaris: Detection of Amplitude Growth". The Astronomical Journal. 135 6: 2240 online hapa
 • Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 437 online kwenye archive.org
 • Turner, D. G.; Kovtyukh, V. V.; Usenko, I. A.; Gorlova, N. I. 2013. "The Pulsation Mode of the Cepheid Polaris". The Astrophysical Journal Letters. 762: L8 online hapa
 • Ptolemys Almagest, translated and annotated by G.J. Toomer, London 1984, ISBN 0-7156-1588-2 online hapa
                                     
 • moyo wa kimama kumuombea muuaji aliyeonekana kukabili adhabu ya kifo bila kutubu Nilitaka kwa gharama yoyote kumzuia asiende motoni milele Nilikuwa na
 • anatukumbusha kuwa yaliyotupata ni matokeo ya dhambi zetu, na kuwa tunapaswa kutubu kwa kushiriki kazi ya Mkombozi. Mwenyewe alizingatia sana fumbo la msalaba:
 • kurithi ufalme mbinguni. Ubatizo: Kubatizwa kwa maji ni sakramenti ya kutubu dhambi na kuzaliwa tena. Ubatizo unafaa kufanywa kwenye maji ya kawaida
 • wazushi na kuwahoji juu ya imani zao. Wakionekana kuwa na makosa wasitake kutubu walikabidhiwa mikononi mwa serikali iliyotoa adhabu ya kifo. Hata hivyo
 • wachungaji na maaskofu waliowahi kuwa dhaifu hiyo walipokelewa tena baada ya kutubu Ndipo Wakristo wa Karthago walio wengi walikataa kuwakubali tena. Wakiongozwa
 • kuhubiri kwamba wasiookoka watateswa milele, kwamba kila mtu anahitaji kutubu na kwamba Mungu anatuwezesha kuwa watakatifu, yaani tukiishi maisha ya
 • za kulitekeleza a. Mwanzo kumuamini Mungu na kumuabudu kumnyenyekea na kutubu kuomba mwanga wake Salamu Maria b. Sala yenyewe mawazo mafupi ya imani kwa

Users also searched:

...
...
...