Back

ⓘ Mapacha (kundinyota)
Mapacha (kundinyota)
                                     

ⓘ Mapacha (kundinyota)

Mapacha iko angani kwenye mstari wa Zodiaki kati ya Kaa pia Saratani, lat. Cancer upande wa mashariki na Ng’ombe Taurus upande wa magharibi.

Inapakana na kundinyota jirani la Kaa Cancer, Pakamwitu Lynx, Hudhi Auriga, Ngombe Taurus, Jabari Orion, Munukero Monoceros na Mbwa Mdogo Canis Minor.

Mapacha - Gemini ni sehemu ya zodiaki maana yake mstari wa ekliptiki unapita humo. Ilhali miendo ya Mwezi na sayari inafuatana karibu na ekliptiki magimba haya huonekana katika eneo la Mapacha kwa wakati fulani kwenye mwaka.

                                     

1. Jina

Mabaharia Waswahili walijua nyota hizi kwa jina la Jauza tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu waliosema جوزاء jawza ambalo linamaanisha mapacha. Waarabu walitafsiri hapa jina la Ptolemaio aliyetaja nyota hizi vile kwa jina la Δίδυμοι didimoi yaani mapacha katika orodha yake ya Almagesti.

Wagiriki wa Kale waliwahi kupokea kundinyota hili likiangaliwa kama mapacha kutoka utamaduni wa Babeli. Hapa ni hasa nyota mbili angavu zaidi za Castor na Pollux zilizotazamamiwa kama vichwa vya watoto mapacha wawili. Katika mitholojia ya Wagiriki kuna hadithi ya malkia Leda aliyekuwa maridadi kiasi cha kumvuta mungu mkuu Zeus kwake. Zeus alimtembelea Leda katika umbo la bata maji tazama pia Dajaja akampa mimba. Leda alilala siku ileile kwa mume wake na kupokea mimba kutoka kwake pia. Wavulana wawili walizaliwa pamoja kama mapacha lakini Pollux alikuwa mwana wa mungu Zeus ilhali Castor alikuwa mwana wa mfalme. Walipendana na kusafiri pamoja kwenye Merikebu ya Argo na mashujaa wakubwa. Castor aliuawa katika mapigano; Pollux ambaye hakuweza kufa kutokana na kuwa nusu-mungu akikuwa na huzuni akamwomba baba Zeus kumwunganisha na kakaye. Hivyo Zeus aliwaweka wote wawili angani kama nyota. Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Jauza" limesahauliwa ikiwa kundinyota linaitwa kwa tafsiri tu "Mapacha".

Gemini - Mapacha ni kati ya makundinyota 48 yaliyotajwa tayari na Klaudio Ptolemaio katika kitabu cha Almagesti wakati wa karne ya 2 BK. Iko pia katika orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia kwa jina la Gemini. Kifupi chake rasmi kufuatana na UKIA ni Gem.

                                     

2. Nyota

Nyota za Mapacha huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Mapacha" inaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.

Kuna nyota 85 katika eneo la kundinyota hili na kuna mbili hasa zinazoonekaka vizuri kwa macho matupu zikikaa karibu na kuwa msingi wa jina la kundi ambazo zinaitwa Castor na Pollux kwa majina ya Kigiriki zilizotazamiwa na watu wa kale kama mapacha mawili. Nyota angavu zaidi ni Pollux inayofuatwa na Castor. Johann Bayer aliziona kwa kosa kinyume hivyo aliandikisha majina ya Alfa Gemininis kwa Castor na Beta Geminis kwa Pollux katika orodha yake.

 • Pollux Beta Geminis ni nyota jitu jekundu yenye mwangaza unaonekana wa 1.2 ikiwa umbali wa miakanuru 34 kutoka dunia. Pollux imegunduliwa kuwa na sayari ya nje inayoizunguka.
 • Castor Alfa Geminis inaonekana kwa darubini kama mfumo wa nyota 6 zinazoonekana kwa macho kama nyota 1 tu. Ina umbali wa miakanuru 52 kutoka dunia. Uangavu unaoonekana ni 1.6.
                                     

3. Marejeo

 • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 222 ff online kwenye archive.org
 • H. A. Rey, The Stars - A New Way To See Them. Enlarged World-Wide Edition. Houghton Mifflin, Boston, 1997. ISBN 0-395-24830-2.
 • Levy, David H. 2005. Deep Sky Objects. Prometheus Books. ISBN 1-59102-361-0.
 • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
 • Ridpath, Ian; Tirion, Wil 2001, Stars and Planets Guide, Princeton University Press, ISBN 0-691-08913-2
 • Ian Ridpath and Wil Tirion 2007. Stars and Planets Guide, Collins, London. ISBN 978-0-00-725120-9. Princeton University Press, Princeton. ISBN 978-0-691-13556-4.
                                     

4. Viungo vya Nje

 • WikiSky: Gemini constellation
 • Astrojan Astronomical Picture Collection: The clickable Gemini
 • Constellation Guide: Gemini constellation
 • Ian Ridpaths Star Tales: Gemini
 • The Deep Photographic Guide to the Constellations: Gemini
 • APOD Pictures of Gemini and Deep Sky Objects
 • The Medusa Nebula
 • Open Star Clusters M35 and NGC 2158
 • The Eskimo Nebula from Hubble
 • NGC 2266: Old Cluster in the NGC
 • A Spring Sky Over Hirsau Abbey
 • Warburg Institute Iconographic Database over 300 medieval and early modern images of Gemini
                                     
 • hizi zina athari kwa kipindi fulani cha mwaka kinachoitwa kufuatana na kundinyota au buruji ya falaki yake. Lakini hali halisi Jua linapita katika maeneo
 • kwa kusudi la kulingana na kalenda ya miezi 12. Kwa kufikia idadi hii kundinyota la Hawaa Ophiuchus liliondolewa katika idadi ya Zodiaki. Kwa jumla majina
 • α Alpha Aurigae, kifupi Alpha Aur, α Aur ni nyota angavu zadi katika kundinyota la Hudhi Auriga Ni pia nyota angavu ya sita kabisa kwenye anga. Mwangaza

Users also searched:

...
...
...