Back

ⓘ Alda
                                     

ⓘ Alda

Alda wa Siena alikuwa mwanamke Mkristo wa Italia.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Aprili.

                                     

1. Maisha

Alda alizaliwa Siena leo mkoani Toscana; baada ya kuishi miaka saba katika ndoa bila kupata mtoto, alifiwa mumewe.

Hapo alitawa upwekeni nje ya mji na kujitosa katika kujinyima na kutoa sadaka.

Baada ya kupata njozi kuhusu Yesu kutenda kama inavyoelezwa na Injili, aligawa mali zake zote akaenda kuishi hospitalini ili kuhudumia wagonjwa. Katika kazi hiyo ilitokea miujiza kadhaa.

Siku moja wahudumu wenzake wasioamini njozi zake, alipokuwa nje ya nafsi yake, walimchoma mwilini kwa sindano na moto, lakini hakuwa na itikio lolote mpaka baada ya kujirudia. Hapo alisema tu kwa unyenyekevu, "Mungu awasamehe", jambo lililomvutia wote.