Back

ⓘ Ukame
Ukame
                                     

ⓘ Ukame

Ukame ni hali ya hewa ya sehemu au mahali fulani inayofanya pakose maji ya kutosha kwa muda mrefu. Kwa kawaida hii inamaanisha kipindi ambako kuna mvua kidogo, au kupungukiwa kwa usimbishaji mwingine kama theluji.

Ukame unatokea pia pale ambako watu na kilimo wanategemea maji kwa umwagiliaji na vyanzo vingine vya maji vinakauka.

Ukame unaweza kuhatarisha uhai wa mimea, wanyama na watu, ambao wote wanahitaji maji.

                                     

1. Matokeo ya ukame

  • lishe ya wanyama inapungua, bei za nyama, maziwa na bidhaa nyingine zinazotokana na wanyama zinapanda
  • usafirishaji wa bidhaa kwenye njia za maji unapata matatizo kama maji mtoni na miferejini yanapungua mno
  • kukausha kwa mimea inaacha ardhi bila kinga, mmomonyoko unaongezeka
  • mavuno yanapungua, bei za mazao yanapanda
  • vituo vya umeme na viwanda ambavyo vinategemea maji ya mito kwa kupoza mashine zao haziwezi kuendelea kwa nguvu; kiasi cha maji kinachopatikana kinapungua, na maji hayo yanakuwa na halijoto ya juu zaidi, kwa hiyo uwezo wa kupoza injini inapungua
  • hatari ya moto kwenye misitu na porini
  • hakuna maji ya kutosha kwa wakazi wa eneo fulani.
  • dhoruba itabeba kiasi kikubwa cha mchanga na vumbi kwenye angahewa, hivyo kupeleka ardhi yenye rutuba penginepo na kuongeza magonjwa ya mfumo wa upumuaji kutokana na vumbi hewani.
  • uzalishaji wa umememaji unapungua kama hakuna maji ya kutosha tena kuendesha rafadha

Users also searched:

...
...
...