Back

ⓘ Madonna (mwanamuziki)
Madonna (mwanamuziki)
                                     

ⓘ Madonna (mwanamuziki)

Madonna Louise Ciccone ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za pop dansi, mwigizaji na mfanyabiashara kutoka nchini Marekani.

Alijipatia umaarufu kwa kuwa na mashairi makali na muonekano wa kuvutia katika video za nyimbo zake ambazo zilipelekea kuwa alama katika MTV. Madonna anajulikana kwa kujibadilisha katika muziki na muonekano, na kwa kudumisha unguli wake katika sekta ya muziki. Wakosoaji wa muziki wamebeza tungo zake, na hivyo kupelekea chuki kwa kiasi fulani. Akijulikana kama "Malkia wa Pop", Madonna mara nyingi anachukuliwa na wasanii wengine kama mtu mwenye ushawishi.

Akiwa amezaliwa Bay Mji, Michigan, Madonna alihamia jiji la New York mwaka 1977 kujiingiza katika ngoma za kisasa. Baada ya kufanya katika makundi ya muziki Breakfast Club na Emmy, alisaini na Sire Records lebo tanzu ya studio ya Warner Bros Records mwaka 1982 na kuachia albamu ya kwanza mwaka uliofuata. Alifuatisha mfululizo wa albamu zilizofanikiwa, ikiwa ni pamoja na ushindi wa Tuzo ya Grammy Ray ya Mwanga 1998 na Confessions on Dance Floor 2005. Katika kazi yake, Madonna ameandika na kurekodi nyingi kati ya kazi zake, na nyingi za hizo kufikia namba moja katika chati mbalimbali: hizi ni pamoja na "Like a Virgin", "Papa Dont Preach", "Like a Prayer", "Vogue", "Take a Bow", "Frozen", "Music", "Hung Up", and "4 Minutes".

Umaarufu wa Madonna uliimarishwa zaidi kwa ushiriki wake katika filamu kama Desperately Seeking Susan 1985, Dick Tracy 1990, na Evita 1996. Wakati filamu ya Evita ikimpatia tuzo ya Golden Globe Award kama mwigizaji bora wa kike, nyingi za filamu zake zilikuwa na mapokeo hafifu.

Madonna amekuwa akitangazwa kama mfanyabiashara, hasa kwa kampuni ya burudani iitwayo Maverick ikiwa ni pamoja na studio ijulikanayo kama Maverick Records. Katika mwaka 2007 alisaini mapatano ya pekee ya dola za Marekani 120 milioni 360 deal na Live Nation, ambayo ilisababisha mapatano ya kurekodi na Interscope Records. Biashara zake nyingine ni pamoja na ubunifu wa mavazi, kuandika vitabu vya watoto, na kutengeneza filamu.

Akiwa ameuza zaidi ya rekodi milioni 300 duniani kote, Madonna ametambuliwa na Guinness World Records kama msanii wa kike mwenye mauzo ya juu wa wakati wote. Recording Industry Association of America RIAA ilimtaja kama mwimbaji wa kike wa muziki wa rock mwenye mauzo ya juu kuliko wote katika karne ya 20 na mwanamuziki wa kike wa pili aliyethibitika katika Marekani akiwa na kopi milioni 64.5. Madonna mwimbaji wa juu zaidi wa peke yake kwa wakati wote, akijipatia dola za Marekani bilioni 1.31 kutoka katika matamasha yake tangu mwaka 1990. Alifanikiwa kuwa mmoja kati ya waanzilishi watano wa jumba la mastaa Uingereza UK Music Hall of Fame na aliingizwa katika Rock na Roll Hall of Fame katika mwaka wake wa kwanza wa uhakiki. Madonna alikuwa katika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya VH ya wanawake 100 nguli katika muziki na namba mbili nyuma tu ya Beatles katika orodha ya Billboard ya wasanii wakubwa 100 wa wakati wote.

                                     

1. Maisha na kazi

1958-1981: maisha na kazi ya mwanzo

Madonna alizaliwa na wazazi Wakatoliki Silvio Anthony "Tony" Ciccone na Madonna Louise Fortin katika mji wa Bay City, Michigan tarehe 16 Agosti 1958. Wazazi wa baba yake walikuwa wahamiaji kutoka Pacentro, Italia, wakati mama yake alikuwa wa asili ya Ufaransa-Canada. Tony alifanya kazi kama mhandisi katika kampuni ya Chrysler na General Motors. Wakati Madonna alikuwa na jina sawa na la mama yake, wanafamilia walizoea kumwita "Little Nonni". Alikuwa na kaka wakubwa wawili, Anthony na Martin, na ndugu wa kike watatu, Paula, Christopher na Melanie.

                                     

2. Tuzo

Amadeus Austrian Music Awards

Madonna ameshinda mara moja na kuteuliwa mara mbili, mnamo 2006.

Billboard Touring Awards

Madonna ameshinda tuzo nne, na kuteuliwa mara nane.

Grammy Awards

Madonna ameshinda tuzo saba, na kuteuliwa mara ishirini na nane.

Hungarian Music Awards

Madonna ameshinda tuzo mara mbili, na kuteuliwa mara sita.

Ivor Novello Awards

Madonna ameshinda mara mbili, na kuteuliwa mara tano.

                                     
  • Love na baadaye alitunga tena kwa ajili ya wasanii maarufu kama vile Madonna Crazy for You Michael Jackson Human Nature The Pointer Sisters
  • kushiriki katika kuandaa nyimbo zao isipokuwa Beyonce Knowles, B Day na Madonna Ijapokuwa Carey aliyamani kufanya kazi na kundi hili lakini haikuwezekana
  • Mariah Carey amezaliwa tar. 27 Machi 1970 ni mwanamuziki mtunzi, mtayarishaji na pia ni mwigizaji wa Kimarekani. Alitengeneza albamu yake iliyofanya
  • mfumo wa kialfabeti inataja orodha ya nyimbo zilizotungwa au kushiriki kutunga na mwanamuziki mtunzi na mtayarishaji kutoka nchini Marekani Babyface.

Users also searched:

...
...
...