Back

ⓘ Ahabu
Ahabu
                                     

ⓘ Ahabu

Ahabu, mwana wa Omri, alikuwa mfalme wa saba katika ufalme wa Israeli. William F. Albright alikadiria utawala wake kuwa miaka 869–850 KK, E. R. Thiele miaka 874–853 KK na Michael D. Coogan miaka 871–852 KK.

Vitabu vya Wafalme vinamchora kama mwovu sana, kwa kufuata mke wake Yezebeli, kumuua Naboti na kuelekeza taifa la Israeli kuabudu miungu mingi, hasa Baali.

Lakini Nabii Elia kwa karama yake ya kutokea na kutoweka hakuweza kuuawa kama manabii wenzake wengi, akafaulu kuokoa imani katika Mungu pekee, YHWH.

Users also searched:

...
...
...