Back

ⓘ Mfereji wa bahari
Mfereji wa bahari
                                     

ⓘ Mfereji wa bahari

Mfereji wa bahari ni kama bonde au korongo kwenye sakafu ya bahari.

Mara nyingi mifereji ya bahari huwa na mitelemko mikali ya kuelekea chini. Huwa mirefu lakini kiasi nyembamba. Urefu unaweza kufikia kilomita 2.400 na upana hadi km 112.

Mfereji wa bahari uliyoenea chini kabisa duniani ni mfereji wa Mariana wenye kina cha mita 11.034 uliopo katika bahari ya Pasifiki kando ya Visiwa vya Mariana karibu na Guam. Ni mahali ambako bamba la Pasifiki hujisukuma chini ya Bamba la Ufilipino.

Kwa jumla mifereji hii inapatikana mahali ambako bamba la gandunia linasukumwa chini ya bamba lingine.

Kwa hiyo mazingira ya mifereji ya bahari yana mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara pamoja na tsunami zinazotokana na mitetemeko hiyo.

Kwenye kona au mipaka ya mifereji ya bahari mara nyingi kuna safu za visiwa vilivyojengwa na volkeno zilizoanza kwenye sakafu ya bahari.

Users also searched:

...
...
...