Back

ⓘ Anjelo wa Acri
Anjelo wa Acri
                                     

ⓘ Anjelo wa Acri

Anjelo wa Acri, O.F.M.Cap. alikuwa padri wa Acri, maarufu kama mhubiri wa Neno la Mungu.

Papa Leo XII alimtangaza mwenye heri tarehe 18 Desemba 1825, halafu Papa Fransisko alimtangaza mtakatifu tarehe 15 Oktoba 2017.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 30 Oktoba.

                                     

1. Maisha

Kabla hajatulia utawani alitoka mara mbili, lakini hatimaye alidumu na kufanya kazi kubwa ya uinjilishaji katika Ufalme wa Sisili mbiliakiongoa watu wengi sana, hata akaitwa "Malaika wa Amani" na "Mtume wa Kusini".

Pia alijulikana kwa sababu ya kujaliwa njozi, kutoka nje ya nafsi mara kadhaa wakati wa Misa, na hata kupatikana mahali pawili kwa wakati mmoja.