Back

ⓘ Mdudu Mabawa-potwa
Mdudu Mabawa-potwa
                                     

ⓘ Mdudu Mabawa-potwa

Wadudu mabawa-potwa ni wadudu wadogo wa oda Strepsiptera wenye mabawa yaliyopotwa. Wadudu hawa ni wadusia wa wadudu wengine, kama nyuki, nyigu, sisimizi, warukaji-majani, mende, panzi na visamaki-fedha.

Madume ya wadudu hawa wana mabawa, miguu, macho na vipapasio kama wadudu wengine, lakini majike wanafanana na lava bila viungo hivi neotenia, Kiing. neoteny. Majike wanakaa katika mdudu ambamo wamezaliwa. Wanatoa kichwa na protoraksi nje ya mwenyeji ili kumrahisishia dume apande jike.

Kuna familia 7 na spishi 110 katika Afrika.

                                     

1. Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki

  • Corioxenos antestiae
  • Halictophagus regina
  • Xenos zavattarii
  • Halictophagus pontifex
  • Halictophagus clodoceras
  • Elenchus eastopi
  • Halictophagus scheveni
  • Coriophagus zanzibarae
  • Halictophagus zanzibarae

Users also searched:

...
...
...