Back

ⓘ Alberto wa Pontida
Alberto wa Pontida
                                     

ⓘ Alberto wa Pontida

Alberto wa Pontida, O.S.B., alikuwa abati huko Lombardia, Italia.

Alberto alikuwa kati ya wamonaki waliojitahidi zaidi kueneza urekebisho wa Cluny katika mkoa huo. Hata hivyo, alikuwa upande wa kaisari Henri IV katika mashindano yake na Papa Gregori VII.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 2 Septemba pamoja na mtakatifu Vitus.

                                     

1. Maisha

Kabla hajajiunga na umonaki, alikuwa askari kufuatana na kawaida ya koo maarufu za wakati huo. Ni baada ya kujeruhiwa sana vitani kwamba aliamua kufuata maisha ya Kiroho.

Alipokwenda kuhiji Santiago de Compostela Hispania alipitia monasteri kadhaa za Waklunii na kuvutiwa sana na maisha ya namna hiyo.

Aliporudi nyumbani alijitolea mali yake kuanzisha monasteri 1059.

Baadaye alikwenda kupata malezi ya Ugo wa Cluny kwa miaka saba.

Tena akarudi Pontida kuongoza monasteri yake na kuanzisha nyingine kwa wanawake.

                                     

2. Marejeo

  • Cognomi e famiglie del bergamasco, S.E.S.A.A.B., Bergamo, 2000
  • J. Huizinga, Lautunno del Medioevo, Newton-Compton, Roma, 1997;
  • J. Le Goff, Luomo medievale, Laterza, Bari, 1999;
  • G.M. Cantarella, I monaci di Cluny, Einaudi, Torino, 1997;