Back

ⓘ Lava (volkeno)
Lava (volkeno)
                                     

ⓘ Lava (volkeno)

Kwa kutaja watoto wa wadudu angalia makala ya lava

Lava kutoka jina la Kiingereza lenye asili ya Kilatini lava, wakati mwingine pia "zaha" ni mwamba ulio katika hali ya kiowevu kutokana na joto kali. Chini ya uso wa dunia mwamba joto wa kuyeyuka huitwa "magma" badala ya lava. Sawa na magma yenyewe lava inaweza kuwa nzito kama ujiuji au nyepesi kama majimaji.

Lava inatoka nje kwa kawaida wakati wa mlipuko wa volkeno. Inaweza kutoka pia katika ufa kwenye ganda la dunia.

Wakati wa kutoka hali yake ni kiowevu yenye halijoto kati ya 600°C hadi 1200°C. Ndani ya shimo la kasoko ya volkeno lava inaweza kukaa kama ziwa la kuchemka.

Ikitoka nje ya kasoko inaweza kuwa kama mto wa moto. Mwendo wake hutegemea na mnato wake yaani kama hali yake ni zaidi majimaji au ujiuji. Kadiri inavyoenea mbali na kasoko inapoa na kuwa mwamba.

Ikipoa inaganda na kuwa mwamba imara.

                                     
  • Mlima Borawli ni mlima wa volikano wenye nyumba za lava uliopo ukanda wa Afar nchini Ethiopia. Upo juu ya pwani ya mashariki mwa ziwa Afrera.
  • wa mashariki wa mlangobahari kuna pia visiwa vilivyojengwa na volkeno zilizomwaga lava chini ya uso wa bahari na kukua juu yake. Visiwa kadhaa visivyo
  • igneous rock yanasaidia kujua umri wa mwamba tangu kuganda kubadilika kutoka lava kuwa mwamba Madini makubwa yanamaanisha mwamba uliopozwa polepole labda
  • yanakutana kuna ufa unaoruhusu kupanda juu kwa magma na lava kutoka koti ya Dunia kama mstari wa volkeno chini ya maji. Miamba hiyo kwenye hali ya kiowevu inaganda
  • Lengai, ikiwapo volkeno hai katika eneo la Serengeti, ni mlima wa moto pekee ambao bado hutoa carbonatite lava Carbonatite lava unapofichuliwa
  • Magharibi mwa Danaki. Una upana wa kilomita 12, tawi la kilele cha volkano. Lava za Basaltiki zinamwagika katika matawi ya Asavyo, yanayounganisha uwanda
  • hayo yanakutana kuna ufa unaoruhusu magma na lava kupanda juu kutoka koti ya Dunia kama mstari wa volkeno chini ya maji. Miamba hiyo yenye hali ya kiowevu

Users also searched:

...
...
...