Back

ⓘ Kirgizia
Kirgizia
                                     

ⓘ Kirgizia

Kirgizia pia Kirgizstan, Kirigizistani au Kigistani ; kwa Kikirgizi: Кыргызстан Kyrghyzstan ; kwa Kirusi: Киргизия Kirgizia) ni nchi ya Asia ya Kati.

Imepakana na Kazakhstan, Uzbekistan, Tajikistan na China.

                                     

1. Historia

Hadi mwaka 1991 Kirgizia ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyet, ikijulikana kwa jina la "Jamhuri ya Kisovyeti ya Kikirgizi".

Ilipata uhuru wake katika mwendo wa kuporomoka kwa Umoja wa Kisovyeti.

Kabla ya uhuru yalitokea mabadiliko katika uongozi wa chama cha kikomunisti. Viongozi wapya waliotafuta njia bila udikteta mkali walishika uongozi na rais Askar Akayev alirudishwa madarakani katika uchaguzi wa kwanza na wa pili.

Lakini uchaguzi wa mwaka 2005 ulionekana haukuwa huru, hivyo hasira ya wananchi ikalipuka katika mapinduzi. Uchaguzi mpya ukamteua mpinzani wa awali Kurmanbek Bakiyev.

                                     

2. Mgawanyo kiutawala

Hii ni orodha ya mikoa ya Kirgizia pamoja na makao makuu yake:

 • Mkoa wa Naryn
 • Bishkek mji
 • Mkoa wa Batken
 • Mkoa wa Chuy Bishkek
 • Mkoa wa Osh Mjini mji
 • Mkoa wa Issyk Kul Karakol
 • Mkoa wa Talas
 • Mkoa wa Jalal-Abad Jalal-Abad
 • Mkoa wa Osh
                                     

3. Wakazi

Idadi ya wakazi ilihesabiwa 2005 kuwa watu 5.264.000. Takriban 72.6 % kati yao ni Wakirgizi wenyewe, ambao ni jamii ya Waturuki halafu kuna Wauzbeki 14.4 % hasa kusini na Warusi 6.4 % hasa kaskazini, mbali na makundi madogo zaidi.

Lugha ya kawaida ni Kikirgizi, ambacho ni lugha rasmi pamoja na Kirusi. Angalia pia orodha ya lugha za Kirgizia.

Takriban 64% ni Waislamu, lakini kuna uhuru wa dini. Wakristo wako hasa katika ya wakazi wenye asili ya Ulaya, wakiwemo kwanza Waorthodoksi, halafu Waprotestanti na Wakatoliki wachache.

                                     

4. Marejeo

 • Kyrgyzstan: The Growth and Influence of Islam in the Nations of Asia and Central Asia by Daniel E. Harmon
 • Kyrgyzstan: Central Asias Island of Democracy? by John Anderson
 • Odyssey Guide: Kyrgyz Republic by Ceri Fairclough, Rowan Stewart and Susie Weldon
 • Politics of Language in the Ex-Soviet Muslim States: Azerbaijan, Uzbekistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Turkmenistan and Tajikistan by Jacob M. Landau and Barbara Kellner-Heinkele. Ann Arbor, University of Michigan Press, 2001. ISBN 978-0-472-11226-5
 • Kyrgyzstan: Traditions of Nomads by V. Kadyrov, Rarity Ltd., Bishkek, 2005. ISBN 9967-424-42-7
 • Lonely Planet Guide: Central Asia by Paul Clammer, Michael Kohn and Bradley Mayhew
 • Historical Dictionary of Kyrgyzstan by Rafis Abazov
                                     

5. Viungo vya nje

Serikali
 • Laws of the Kyrgyz Republic
 • Tovuti rasmi ya serikali
 • President of Kyrgyzstan official site
 • Parliament of Kyrgyzstan official site
General information
 • Kigezo:Wikivoyage-inline
 • Kyrgyzstan entry at The World Factbook
 • Kyrgyz Publishing and Bibliography Archived Aprili 5, 2010 at the Wayback Machine.
 • Kyrgyzstan at UCB Libraries GovPubs
 • Country Profile from BBC News
 • Key Development Forecasts for Kyrgyzstan from International Futures
Ramani Wikimedia Atlas of Kyrgyzstan
                                     
 • Bees for Development inaendesha miradi Uganda, Zanzibar, Ethiopia na Kirgizia Ofisi zake ziko Monmouth, Wales Kusini. Ilianzishwa mwaka wa 1993, inafanya
 • kuvamia Ulaya, Uajemi na Uhindi. Kiasili walitokea katika maeneo kati ya Kirgizia na Mongolia ya leo. Hakuna uhakika kuhusu utamaduni na lugha yao. Wataalamu
 • Nouakchott, Mauritania Ngamia wakifanya kazi ya msafara Ngamia nundu - mbili huko Kirgizia Mwenyeji wa Turkmenistan akipanda ngamia yake mnamo 1905 1915 Ngamia wawili
 • Israel Jamhuri ya China Taiwan Japani Kamboja Kazakhstan Kirgizia Korea Kaskazini Korea Kusini Kupro2 Kuwait Laos Lebanoni
 • rahisi zaidi kupandwa juu ya m 7500 Jengish Chokusu Tomur Feng m 7, 439 Kirgizia - China - wa juu katika Tian Shan Qurnat as Sawda m 3, 088 wa juu nchini
 • Israel Jamhuri ya China Taiwan Japani Kamboja Kazakhstan Kirgizia Korea Kaskazini Korea Kusini Kupro2 Kuwait Laos Lebanoni
 • Israel Jamhuri ya China Taiwan Japani Kamboja Kazakhstan Kirgizia Korea Kaskazini Korea Kusini Kupro2 Kuwait Laos Lebanoni

Users also searched:

...
...
...