Back

ⓘ Mdudu Mabawa-makubwa
Mdudu Mabawa-makubwa
                                     

ⓘ Mdudu Mabawa-makubwa

Wadudu mabawa-makubwa ni wadudu wakubwa kiasi hadi wakubwa sana wa oda Megaloptera ambao wana mabawa makubwa yakilinganishwa na mwili wao. Wanaruka angani vigoigoi. Muda wa maisha ya wadudu wapevu ni mfupi, kwa kawaida siku chache. Kwa kinyume lava huishi miaka 1-5 majini.

Oda hii ina familia mbili tu na spishi 8 zimeelezwa katika Afrika. Spishi kubwa kabisa duniani imefunuliwa huko Uchina. Haijapata jina la kisayansi lakini jina la Kiingereza ni Giant dobsonfly. Urefu wa mabawa pamoja ni sm 21.

                                     

1. Spishi za Afrika

  • Madachauliodes ranomafana
  • Taeniochauliodes ochraceopennis
  • Leptosialis necopinata
  • Platychauliodes woodi
  • Leptosialis africana
  • Platychauliodes capensis
  • Chloroniella peringueyi
  • Madachauliodes torrentialis

Users also searched:

...
...
...