Back

ⓘ Paulo Burali
Paulo Burali
                                     

ⓘ Paulo Burali

Paulo Burali wa Arezzo alikuwa askofu mkuu wa Napoli na kardinali kutoka shirika la Wateatini.

Ujuzi wake wa sheria ulimpa vyeo vikubwa katika mahakama za Napoli pamoja na nafasi za kutetea haki za wananchi.

Hata hivyo aliacha kila kitu ili kufuata wito wake wa kitawa. Alipewa upadrisho tarehe 26 Machi 1558.

Baada ya kushika uongozi shirikani, Papa Pius V alimfanya kardinali tarehe 17 Mei 1570, halafu chini ya Papa Gregori XIII alipewa askofu tarehe 4 Julai 1572 akaongoza jimbo kuu la Napoli miaka 1576-1578.

Pamoja na ukali wake, alichangia sana urekebisho wa Kikatoliki nchini Italia.

Papa Klementi XIV alimtangaza mwenye heri tarehe 18 Juni 1772.

                                     

1. Marejeo

  • Paolo Burali Catholic-Hierarchy
  • Giovanni Bonifacio Bagata, CR, Vita del Venerabile Paolo Burali dArezzo Verona 1698.
  • Andrea Avellino, Brevi cenni sulla vita del Beato Paolo Burali dArezzo seconda edizione Napoli 1876.
  • G. B. Maffi, Vita del Beato Paolo d Arezzo Piacenza 1833.
  • Piacenza e il B. Paolo Burali: atti del convegno di studio in occasione del IV centenario dalla morte Deputazione di storia patria per le province parmensi, 1979.
  • G. B. Bonaglia, Vlta del Beato Paolo Burali d Arezzo, Chierico Regolare, Cardinale di S. Pudenziana Napoli 1772.
  • Epistolario del beato Paolo Burali: cardinale teatino, vescovo di Piacenza, arcivescovo di Napoli 1511-1578 Brescia: Centro bresciano di iniziative culturali, 1977.
  • Biography Salvador Miranda