Back

ⓘ Mdudu Mabawa-marefu
Mdudu Mabawa-marefu
                                     

ⓘ Mdudu Mabawa-marefu

Wadudu mabawa-marefu ni wadudu wadogo wa oda Mecoptera katika nusungeli Pterygota. Familia muhimu za oda hii ni Panorpidae na Bittacidae.

Mabawa ya wadudu hawa ni membamba na marefu yenye vena nyingi zinazoikizika, kama yale ya wadudu siku-moja. Jenasi kadhaa zina mabawa madogo sana au zimepoteza mabawa kabisa.

Mwili vilevile ni mwembamba na mrefu. Fumbatio ya madume inafanana na mkia wa nge: imepindika juu na ncha yake ina umbo lililopapulika ambalo lina uchi wa kiume ndani yake.

Sehemu za kinywa za wadudu hawa ni sahili. Mandibuli ni ndefu zenye pedipalpi nene. Hukamata arithropodi wadogo au hula mizoga.

Lava wa wadudu mabawa-marefu wanafanana na viwavi wenye miguu sita mifupi ya kweli na miguu kadhaa ya bandia. Pingili ya kumi inabeba kisahani cha mfyonzo au jozi ya vikulabu. Hula maada ya mimea au wadudu waliokufa, pengine hukamata wadudu. Lava hugeuka kwa bundo katika udongo au ubao unaooza.

Users also searched:

...
...
...