Back

ⓘ Bahari ya Barents
Bahari ya Barents
                                     

ⓘ Bahari ya Barents

Bahari ya Barents ni tawi la Bahari ya Aktiki, na iko kaskazini kwa Urusi, Norwei na funguvisiwa la Svalbard pamoja na Kisiwa cha Dubu. Visiwa vya Novaya Zemlya vinaitenganisha na Bahari ya Kara.

Eneo lake ni la km² 1.424.000. Jina limetokana na baharia Mholanzi Willem Barents.

Sehemu hii ya bahari haina kina kirefu, kwa wastani ni mita 230 pekee. Kiuchumi ni muhimu kwa uvuvi na uchumbaji wa gesi na mafuta ya petroli.

Hata kama ni sehemu ya Bahari ya Aktiki, inaweza kupitiwa na meli karibu mwaka wote kwa sababu inapokea maji ya vuguvugu kutoka Mkondo wa Ghuba wa Bahari Atlantiki unaoishia hapa. Maji ya vuguvugu ni msingi kwa kuota kwa planktoni ambayo ni lishe kwa aina nyingi za samaki.

Users also searched:

...
...
...