Back

ⓘ Mashimo ya Ajabu Duniani
                                     

ⓘ Mashimo ya Ajabu Duniani

Mashimo ya ajabu duniani ni kama yafuatayo na mengine mengi.

  • Bingham Canyon##

Shimo la Bingham Canyon lipo katika machimbo ya shaba yaliyo katika milima ya Oquirrh, Utah, Marekani. Shimo hilo lenye urefu wa kilometa 2 na upana wa kilometa 4 ni moja kati ya mashimo ya ajabu yaliyotengenezwa na watu.

  • Mirny##

Shimo hilo liko katika Machimbo ya Almasi yanayopatikanika Siberia katika Mgodi wa Mirny. Shimo hili lina urefu wa mita 525 na upana wa mita 1200.

  • Great Blue##

Shimo hili linajulikana kama Great Blue hole. Shimo hili lipo chini ya maji kwenye Ufukwe wa Belize, lina upana wa futi 1000 na urefu wa futi 400. Shimo hili linatokana na Pango la barafu lililokuwepo sehemu hiyo.

  • Shimo la gesi la Darvaza##

Shimo hili liligunduliwa mwaka 1971 barani Asia katika nchi ya Turkmenistan. Wataalamu wa miamba waligundua mlundikano mkubwa wa gesi katika ardhi ya eneo hilo. Hivyo waliamua kuchimba ili kuifikia. wakiwa katika uchimbaji ghafla eneo hili likaachia na kutokea shimo kubwa lenye gesi. Katika kuikinga gesi hiyo, inayoaminika kuwa na sumu ya kudhuru watu, wataalamu hao waliiunguza, hivyo siku zote shimo hilo limekuwa likiwaka moto.

  • Kimberley##

Shimo la Kimberley lililotokana na machimbo ya almasi yaliyopo Afrika Kusini. Pia linafahamika kuwa shimo kuu tangu mwaka 1886 hadi mwaka 2014. Shimo hili lilikuwa likishika nafasi ya 50.000 shimo hili liliweza kutoa almasi yenye kilogramu 2.722 kwa mwaka. Ni miongoni mwa mashimo yaliyo katika orodha ya urithi wa Dunia.

  • Sinkhole##

Mwaka 2007 shimo hili lenye urefu wa futi 300 lilipoteza maisha ya watu wawili. Nyumba kadhaa zilidondokea ndani yake. Pia shimo hili lilisababisha maelfu ya watu kukosa makazi. Shimo hili lilisababishwa na mvua pamoja na mkondo wa maji uliopita chini ya ardhi.

  • Diavik##

Shimo hili lipo upande wa kaskazini magharibi mwa nchi ya Canada katika mgodi wa Diavik ukiwa umeanzishwa mwaka 2003. Mgodi huu uzalisha kilo 1600 za almasi kila mwaka.

Users also searched:

...
...
...