Back

ⓘ Rasi Hoorn
Rasi Hoorn
                                     

ⓘ Rasi Hoorn

Rasi Hoorn ni rasi katika Chile kwenye sehemu ya kusini kabisa ya Amerika Kusini. Ni mahali ambako maji ya Pasifiki na maji ya Atlantiki hukutana.

Jina linatokana na mji wa Hoorn katika Uholanzi, kwa sababu walikuwa mabaharia kutoka mji ule waliochora rasi hii kwenye ramani mara ya kwanza na kuiteulia jina.

Rasi Hoorn ni ncha ya kusini ya funguvisiwa la Tierra de Fuegos kwa Kiingereza fireland ambavyo ni kundi la visiwa linalozunguka sehemu ya kusini ya Amerika Kusini bara.

Kabla ya kujengwa kwa Mfereji wa Panama njia ya rasi Hoorn ilikuwa njia muhimu kwa meli kati ya bahari mbili. Mizigo mingi iliyoelekea Kalifornia, Chile au Peru ilipita huko au kwenye mlangobahari wa Magellan uliopo takriban kilomita 120 upande wa kaskazini.

Rasi Hoorn ilitazamwa kuwa hatari kutokana na baridi, dhoruba kali, ukungu wa mara kwa mara, mkondo wa bahari na kutokea kwa siwa barafu kutoka Antaktiki. Zaidi ya meli na jahazi kubwa 800 ziliharibika huko kwa kuzama au kugonga miamba, na watu zaidi ya 10.000 walikufa katika ajali hizo. Ndiyo sababu ikaitwa "makaburi ya mabaharia".

Leo hii usafiri wa mizigo unapita katika mfereji wa Panama.

                                     

1. Viungo vya nje

 • Robert FitzRoys commemorative plaque in Horn Island image Archived Oktoba 21, 2010 at the Wayback Machine.
 • International Association of Cape Horners
 • Adventurer George Kourounis expedition to Cape Horn
 • Cape Horn, Tierra Del Fuego, Antarctica and South Georgia Archived Machi 19, 2006 at the Wayback Machine. - antique charts of the Cape Horn region
 • Sailing Way Down South – Ellen MacArthurs rendezvous at Cabo de Hornos
 • Ramani ya bahari iliyotengenezwa na HMS Beagle, 1830–1834; National Maritime Museum, Greenwich Archived Agosti 11, 2004 at the Wayback Machine.
 • A monument at the end of the world Archived Februari 7, 2012 at the Wayback Machine. - Chilean sculptor José Balcells article Spanish
 • Taarifa ya safari ya Jacob Le Maires mnamo 1621 pamoja na ramani na picha
 • Ramani na wakazi asilia National Library of Australia
 • Satellite image and infopoints Archived Septemba 18, 2010 at the Wayback Machine. on BlooSee
 • Chilean Brotherhood of Cape Horn Captains Caphorniers

Users also searched:

...