Back

ⓘ Madonda matakatifu
Madonda matakatifu
                                     

ⓘ Madonda matakatifu

Madonda matakatifu ni jina linalotumiwa na Wakristo kutaja majeraha au maumivu katika viungo vya mwili ambapo Yesu alipatwa na madonda 5 wakati wa kusulubiwa, yaani mikono, miguu na ubavu, lakini pia kichwa na sehemu nyingine alipotiwa taji la miiba au kupigwa mijeledi.

Mtume Paulo mwishoni mwa Barua kwa Wagalatia aliandika, "Mimi nachukua mwilini mwangu chapa stigmata za Yesu." kama zile zinazotiwa juu ya mwili wa wanyama au watumwa ili kutambua ni mali ya nani. Inafikiriwa kwamba alikuwa anadokeza alama za mapigo aliyoyapata kwa ajili ya imani yake.

Watu waliopata alama za namna hiyo lakini bila mapigo ya kawaida walitokea hasa katika watawa wa Kanisa Katoliki kama vile Wadominiko na Wafransisko.

Wa kwanza kujulikana ni shemasi Fransisko wa Asizi. Padri wa kwanza ni Pio wa Pietrelcina.

Asilimia 80 ni wanawake.

                                     

1. Marejeo

 • Living Miracles - Stigmata, Zentropa Real ApS. & Wonders Unlimited, 2005.
 • Boyle, Alan, Science replays the crucifixion, MSNBC, 2005.
 • Carroll, Robert Todd, The Skeptics Dictionary, Wiley, 2003.
 • The Catholic Encyclopedia The Encyclopedia Press, 1913, Online Edition 2003, K. Knight.
 • Sadaputa Dasa, Religion and Modern Rationalism: Shifting the Boundary Between Myth and Science, ISKCON Communications Journal #1.2, July/December 1993.
                                     
 • zikiwemo njozi, kutoka nje ya nafsi na, akiwa na umri wa miaka 29, madonda matakatifu pamoja na kuteswa na shetani. Alitangazwa na Papa Fransisko kuwa
 • Wastigmatini kutoka jina la Shirika la Madonda Matakatifu ambayo kwa Kilatini yanaitwa Stigmata ni shirika la kitawa la kikleri la Kanisa Katoliki.
 • mambo mbalimbali yaliyokuja kutokea kweli baadaye. Pia alijaliwa madonda matakatifu na kupatwa na mateso makali kila Ijumaa na siku zote za Kwaresima
 • karama ya Fransisko wa Asizi. Kanisa Katoliki linakubali ukweli wa madonda matakatifu aliyosema alikuwanayo tangu tarehe 5 Aprili 1697 hadi kifo chake.
 • maisha yake. Inasemekana kuwa tarehe 1 Aprili 1375 huko Pisa alijaliwa madonda matakatifu yasiyoonekana hadi kifo chake. Baada ya majaribio mengi, hatimaye
 • mshangao wenye furaha nd. Elia Bombarone alipowaandikia juu ya ajabu la madonda matakatifu mwilini mwake lililobaki siri kwa wote, isipokuwa wachache. Ajabu
 • asiendelee kusafiri sana kwa ajili ya utume. Hasa baada ya kutiwa madonda matakatifu akaja kuhitaji mfululizo ndugu wauguzi ambao wakawa hivyo mashahidi

Users also searched:

...
...
...