Back

ⓘ Kiroboto
Kiroboto
                                     

ⓘ Kiroboto

Viroboto ni wadudu wadogo wa oda Siphonaptera. Sehemu za kinywa zimeungana katika kimrija kitumikacho kudunga ngozi na kufyonza damu.

Wadudu hao hawana mabawa, lakini wanaweza kuruka mbali sana ikilinganishwa na ukubwa wao. Kiroboto wa binadamu anaweza kuruka juu sm 18 na mbele sm 33 sawa na m 90 ikiwa mtu wa m 1.8 angaliweza kuruka kama kiroboto.

Viroboto wanaweza kurithisha magonjwa, k.m. tauni hurithishwa na Kiroboto wa Panya.

                                     

1. Spishi zinazojulikana sana

  • Ctenocephalides canis, Kiroboto wa Mbwa Dog flea
  • Ctenocephalides felis, Kiroboto wa Paka Cat flea
  • Pulex irritans, Kiroboto wa Binadamu Human flea
  • Xenopsylla cheopis, Kiroboto wa Panya Tropical rat flea

Users also searched:

...
...
...