Back

ⓘ Bamba la Amerika ya Kaskazini
Bamba la Amerika ya Kaskazini
                                     

ⓘ Bamba la Amerika ya Kaskazini

Bamba la Amerika ya Kaskazini ni kati ya mabamba makubwa ya gandunia ya dunia yetu. Lipo chini ya bara la Amerika ya Kaskazini pamoja na Greenland ikielekea upanda wa mashariki hadi mgongo kati wa Atlantiki na upande wa magharibi hadi Japani na milima ya safu ya Cherskiy katika Siberia.

Chini ya Atlantiki linaachana na bamba la Afrika na bamba la Ulaya-Asia na mstari huu ni mahali pa sehemu ya kaskazini ya mgongo kati wa Atlantiki.

Upande wa kusini linakutana na mabamba madogo ya Karibi na Cocos.

Mpaka wa magharibi hufuata mstari wa pwani la Amerika ya Kaskazini kwa kupakana na bamba la Pasifiki hadi pinde la visiwa vya Aleuti. Mpaka huu umesababisha katika kaskazini-magharibi kutokea kwa visiwa vya Aleuti na pia visiwa vya Kurili kati ya Siberia na Japani.

Users also searched:

...
...
...