Back

ⓘ Mdudu mabawa-manyoya
Mdudu mabawa-manyoya
                                     

ⓘ Mdudu mabawa-manyoya

Wadudu mabawa-manyoya ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa oda Trichoptera katika nusungeli Pterygota. Jina lao ni tafsiri ya jina la kisayansi. Wadudu hawa wanafanana na nondo wadogo na oda hizi zina mnasaba. Lakini badala ya vigamba vya mabawa ya Lepidoptera mabawa ya Trichoptera yanabeba manyoya.

Lava wa spishi nyingi huishi majini lakini wale wa familia Limnephilidae huishi kwenye ardhi. Wanatoa hariri ili kuitengenezea utando au kipeto. Wanaotengeneza utando huishi katika maji yanayotiririka. Utando ni kimbilio na inafaa kutega chakula. Kipeto cha lava wengine wadudu-kipeto kinatumikia kwa kukinga kiwiliwili chororo dhidi ya adui na kinashirikisha vitu vigumu kama chembe za mchanga, vijiti, koa n.k. Lava anaweza kutoa kichwa na kidari toraksi na kutembea akivuta kipeto. Kuna lava ambao huishi majini bila utando au kipeto. Hawa hutumia hariri tu ili kutengeneza kifukofuko cha bundo.

Users also searched:

...
...
...