Back

ⓘ Kuhara
Kuhara
                                     

ⓘ Kuhara

Kuhara au kuendesha ni hali ya kupata choo chepesi au cha majimaji angalau mara tatu kwa siku. Kwa kawaida hudumu kwa siku chache na inaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini kwa sababu ya ukosefu wa maji. Ishara za upungufu wa maji mwilini kwa kawaida huanza na ukosefu wa kunyooka kwa kawaida kwa ngozi na mabadiliko katika tabia za mtu. Hii inaweza kuendelea na kusababisha upungufu wa mkojo, upungufu wa rangi ya ngozi, a mpigo wa haraka wa moyo, na upungufu wa mwitikio inapoendelea kuwa mbaya zaidi. Hata hivyo, huenda kinyesi chepesi lakini kisicho cha majimaji katika watoto wanaonyonya, kikawa cha kawaida.

Sababu kuu ya maambukizo ya matumbo huwa ni kwa sababu ya kvirusi, bakteria, kimelea, au hali inayojulikana kama gastroenteritis. Maambukizo haya kwa kawaida hupatikana kutokana na chakula au maji ambayo yameambukizwa na kinyesi, au moja kwa moja kutoka kwa mtu mwingine ambaye ameambukizwa. Huenda ikagawanywa kwa aina tatu: kuhara maji kwa muda mfupi, kuhara damu kwa muda mfupi, na ukiwa utadumu kwa zaidi ya wiki mbili, kuhara kunaoendelea. Kuhara maji kwa muda mfupi huenda kukasababishwa na maambukizo ya kipindupindu. Ikiwa kuna damu inajulikana kama kuhara. Kuna sababu kadhaa zisizo za kuambukizwa ambazo zinaweza pia kusababisha kuhara ikiwa ni pamoja na: hyperthyroidism, kutovumilia laktosi, ugonjwa wa kuvimba matumbo, baadhi ya dawa, na ugonjwa wa matumbo yanayowashwakati ya sababu nyingine. Katika visa vingi uchunguzi wa kinyesi hauhitajiki ili kuthibitisha sababu halisi.

Unaweza kuzuia kuhara kunaoweza kuambukizwa kwa usafi ulioboreshwa, maji masafi ya kunywa, na kunawa mikono. Kunyonyesha kwa angalau miezi sita kunapendekezwa hata pia chanjo dhidi ya rotavirus. Dawa ya maji ya kunywa ORS, ambayo ni maji masafi yenye viwango vinavyofaa vya chumvi na sukari, ndio matitabu yanayopendekezwa. Tembe za Zinki zinapendekezwa pia. Matibabu haya yamekadiriwa kuwa yamewaokoa watoto milioni 50 kati ya miaka 25 iliyopita. Wakati watu wanahara inapendekezwa kwamba waendelee kula chakula chenye afya na watoto waendelee kunyonya. Ikiwa ORS ya kuuzwa hazipatikani, suluhisho za nyumbani zinaweza kutumiwa. Kwa wale wanoendesha sana, maji ya kudungwa ndani ya venayanaweza kuhitajika. Hata hivyo, katika visa vingi, inaweza kudhibitiwa vizuri kwa maji mdomoni. Viua wadudu, ijapokuwa haitumiwi sana, inaweza kupendekezwa katika visa vichache kama wale wanaohara damu na wana joto jingi, kuhara kunaotokana na kusafiri, na wale wanaopata bakteria au vimelea fulani katika kinyesi chao. Loperamide inaweza kusaidia kupunguza kuhara lakini haipendekezwi kwa wale wenye maradhi makali.

Karibu visa bilioni 1.7 hadi 5 za kuhara hufanyika kila mwaka. Vimekita mizizi sana katika nchi zinazokua, ambapo watoto wadogo wanahara karibu mara tatu kwa mwaka. Duniani kote, hadi 2012, ilikuwa sababu ya pili kuu ya watoto kufariki wakiwa chini ya miaka 5 milioni 0.76 au 11%. Matukio ya mara kwa mara ya kuhara huwa sababu kuu ya utapiamlo na sababu kuu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano. Matatizo mengine ya muda mrefu ambayo yanaweza kutokea ni pamoja na ukuaji duni wa kimwili na kiakili.

                                     
  • Malaria, Kichomi, Magonjwa ya Koo na mapafu, upungufu wa damu, magonjwa ya kuhara magonjwa ya akina Mama, Ajali, kichocho na UKIMWI. Sekta hii ya Afya ina
  • aliyekufa wala viowevu vya mwili wake: damu, matapishi, mkojo, kinyesi au kuhara Nawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni iwapo huwezi kunawa, pangusa
  • vizuizi vya protisi. Dalili zingine zinazotokea mara nyingi hujumuisha: kuhara na ongezeko la hatari ya ugonjwa wa moyo na mishipa. Hata hivyo, athari
  • mwaka Magonjwa ya njia za pumzi milioni 3.9 UKIMWI milioni 2.8 Magonjwa ya kuhara milioni 1, 8 Kifua kikuu milioni 1, 6 Malaria milioni 1, 3 Surua morbilli
  • kudhuru mnyama kimelea. Aina hizi zenye madhara kawaida husababisha wimbi la kuhara ambayo ni kero katika watu wazima na mara nyingi ni hatari kwa afya ya watoto
  • vichangiapo ni pamoja na: Mazoea ya utumbo yasiyojirudia kufungika kwa choo au kuhara ukosefu wa mazoezi, visababishi vya lishe chakula kilicho na kiwango
  • kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa yanayowaathiri watoto kama vile kuhara na nimonia kwa asilimia 50. Mtaji wa binadamu, kwa kupitia elimu, ni kipengee
  • Ugonjwa wa akili Ugonjwa wa Klinefelter Ugonjwa wa kuambukiza Ugonjwa wa Kuhara Ugonjwa wa kupooza Ugonjwa wa malale Ukahaba Ukambi Ukeketaji Ukimwi Ukoma
  • rapid throat test. Kama mtu ana homa na uchungu kwa koo na kukohoa, mafua, kuhara na hisia ya macho mekundu yanayowasha, huenda ikawa ni uchungu wa koo ambayo
  • dawa asilimia 1 ya wagonjwa zinazohusika na matumizi ya Penisilini ni kuhara hypersensitivity, kuhisi kutapika, vipele, neurotoxicity, urticaria na maambukizi

Users also searched:

choo cha mtoto mchanga, dalili za amoeba, dawa ya kuharisha, dawa ya kusafisha tumbo,

...
...
...