Back

ⓘ Mbawakawa
Mbawakawa
                                     

ⓘ Mbawakawa

Mbawakawa ni jina la kawaida la wadudu wadogo hadi wakubwa ya oda Coleoptera. Majina mengine yanayotumika ni mende na kombamwiko, lakini kwa kuwa majina haya hutumika pia kwa wadudu wa oda Blattodea, ni bora kutumia mende-kibyongo na kombamwiko-kibyongo.

Kwa kawaida kiunzi nje cha wadudu hawa ni kigumu sana. Hata mabawa ya mbele yamekuwa kama magamba magumu na pengine magamba haya yameungika kwa kuwa moja. Kiunzi kigumu hiki kinazuia mbuai wadogo wasiwale mbawakawa. Sehemu za kinywa ni sahili lakini spishi mbuai zina mandibuli kubwa na kali mara nyingi. Macho yao yameunda kwa sehemu nyingi kama wadudu wote lakini macho ni madogo kwa kulinganisha na kichwa kuliko wadudu wengi wengine.

Oda ya Coleoptera ni kubwa kuliko oda zote za wanyama ina zaidi ya spishi 400.000. Spishi nyingi bado hazijafafanuliwa na wataalamu wanakisia kwamba jumla ya spishi itazidi milioni moja na kwamba 25% ya spishi zote za wanyama ni Coleoptera. Kwa sasa karibu na 40% ya spishi za nyama zilizofafanuliwa ni Coleoptera. Lakini karibuni hivi wanasayansi wameanza kumaizi kwamba oda hii si monofiletiki, yaani haina mhenga mmoja tu. Nusuoda ya Adephaga inaweza kuwa oda na labda makuni mengine ya Coleoptera yatapewa oda zao.

Kuna majina mbalimbali kwa makundi ya mbawakawa, kama vile: bungo, dundu, fukusi, kidungadunga, kimetameta/kimulimuli, kipukusa, kisaga, mdudu-kibibi, sururu na tuta.

Users also searched:

...
...
...