Back

ⓘ Maangamizi ya Waarmenia
Maangamizi ya Waarmenia
                                     

ⓘ Maangamizi ya Waarmenia

Maangamizi ya Waarmenia maarufu kwa Kiingereza kama Armenian Holocaust, Armenian Massacres na kwa Kiarmenia Մեծ Եղեռն, Medz Yeghern, "Ovu kubwa"), yalikuwa sera ya Dola la Osmani ya kukomesha Waarmenia wote walioishi ndani ya eneo la dola hilo (leo nchini Uturuki.

Makadirio ya waliouawa ni kati ya watu milioni 1 na 1.5.

Tarehe inayohesabiwa kuwa mwanzo wa hayo mauaji ya kimbari ni 24 Aprili 1915, ambapo watawala Waturuki waliteka wasomi Waarmenian 250 mjini Istanbul. Tarehe hiyohiyo miaka 100 baadaye yalifanyika maadhimisho makubwa katika nchi mbalimbalimbali, hasa huko Etchmiadzin, makao makuu ya kiroho ya Waarmenia, ambapo Patriarki Katolikosi Karekin II aliwatangaza kwa jumla waliouawa kuwa watakatifu wafiadini.

Maangamizi yalitekelezwa kwa awamu mbili: kwanza wanaume wazima waliuawa mara moja au kulazimishwa kufanya kazi za shokoa, halafu wanawake, watoto, wazee na wagonjwa waliswagwa na wanajeshi hadi jangwa la Syria ili wafe njiani, baada ya kunyimwa chakula, maji, mbali ya kuibiwa, kubakwa na kuuawa.

Makabila mengine pia, hasa ya Kikristo, kama vile Waashuru na Wagiriki, waliangamizwa na Waturuki wakati huohuo.

Mtawanyiko wa Waarmenia duniani unatokana kwa kiasi kikubwa na mauaji hayo.

Vilevile ni kutokana nayo kwamba Raphael Lemkin alitunga neno genocide mwaka 1943 kama maangamizi ya halaiki ya mpango na kadiri ya sera.

Maangamizi hayo yanahesabiwa ya kwanza katika karne ya 20 yakifuatwa na yale makubwa zaidi ya maangamizi makuu dhidi ya Wayahudi wa Ulaya chini ya Adolf Hitler.

Uturuki, ulioshika nafasi ya Dola la Osmani, unazidi kukataa neno genocide kuhusiana na mauaji ya Waarmenia, ingawa wataalamu wengi wa historia wanaliona kuwa sahihi na nchi nyingi zaidi na zaidi zinaudai ukiri kosa na kupatana na Waarmenia.

                                     

1. Viungo vya nje

 • "Armenians 1915", Armenian Genocide Research Center World Wide Web log, Google Bogger.
 • The Forgotten, videos of interviews with survivors.
 • Genocide, AM.
 • Tavernise, Sabrina, "Armenian Genocide", The New York Times collected news and coverage.
 • Armenian National Institute, Washington, D.C.
 • Pope John Paul II and Pope Francis on the Armenian Genocide
 • "Fall of the Ottoman Empire", Online Encyclopedia of Mass violence chronological index & articles.
 • Armenian Genocide Debate.
 • "Screamers", You tube video documentary, Google, about genocide, featuring System of a Down.
 • The Armenian Genocide Institute-Museum, Yerevan, AM.
                                     
 • ya Dola la Osmani hadi Afrika na Ulaya. Kilele chake kilikuwa maangamizi ya Waarmenia wakati wa vita vya kwanza vya dunia, ambapo waliuawa zaidi ya milioni
 • ya Dola la Osmani hadi Afrika na Ulaya. Kilele chake kilikuwa maangamizi ya Waarmenia wakati wa vita vya kwanza vya dunia, ambapo waliuawa zaidi ya milioni
 • ya Patriarki Katoliki wa Waarmenia Bzoummar, Lebanon Mandhari ya jumla ya makao makuu pamoja na konventi yake Ukumbusho wa Maangamizi ya halaiki ya Waarmenia
 • Waarmenia kuwa walitaka kubomoa milki ya Osmani yalikuwa msingi kwa Maangamizi ya Waarmenia ya miaka 1915 - 1918 Mashtaka dhidi ya Wayahudi wa karne za 19 na 20
 • Kutoka huko wanaongoza Waarmenia milioni 7 hivi waliosambaa duniani hasa baada ya maangamizi ya halaiki yaliyofanywa na Waturuki baada ya Vita Vikuu vya kwanza
 • Mauaji ya kimbari ni maangamizi ya mpango ya kundi zima la watu au ya sehemu yake kwa msingi wa taifa, kabila, rangi au dini. Ingawa ufafanuzi fasaha haujapatikana
 • monasteri ya Kiarmenia kwenye kisiwa cha Akdamar. Tangu maangamizi ya Waarmenia taifa hilo halipo tena hapa lakini watalii wengi Waarmenia wanatembelea

Users also searched:

...
...
...