Back

ⓘ Majira ya baridi
Majira ya baridi
                                     

ⓘ Majira ya baridi

Majira ya baridi ni mojawapo kati ya majira manne ya kanda za wastani, na halijoto yake ni ya baridi kuliko majira mengine. Ni kinyume cha majira ya joto au chaka.

Pengine baridi inakuwa kali sana na kuendana na barafuto: ndiyo maana maeneo mengine ya dunia hayana wakazi wa kudumu, hasa bara la Antaktiki.

Yanafuata majira ya kupuputika majani kwa Kiingereza Fall au Autumn na kutangulia majira ya kuchipua kwa Kiingereza Spring.

Majira hayo yanatokea duniani kwa nyakati tofauti kadiri eneo husika lilivyo kaskazini au kusini kwa ikweta. Hata katika nchi ileile, kwa mfano Kenya, majira ni tofauti upande huu na upande huu wa ikweta.

Majira hayo tofauti hupatikana zaidi katika ukanda wa tropiki.

                                     

1. Wanyama, mimea, binadamu na majira ya baridi

Ili kuhimili ukali wa majira ya baridi, wanyama wengi wana njia mbalimbali za kimaumbile na kitabia.

 • Uhamaji ni mbinu mojawapo inayotumiwa hasa na ndege wakati wa baridi. Hata hivyo, ndege wengi hawahami. Baadhi ya vipepeo pia huhama msimu huu.
 • Wanyama wengine hulala ili kupunguza shughuli metaboli mwilini wakati wa majira ya baridi. Wanyama hao, kama vile vyura, nyoka, na popo huamka msimu huu unapomalizika.
 • Wanyama wengine huhifadhi chakula watakachokula wakati wa majira ya baridi.
 • Wanyama wengine huishi majira ya baridi lakini hujibadilisha kama vile rangi. Rangi ya manyoya hubadilika kuwa nyeupe ili kufanana na theluji. Mifano ya wanyama hawa ni kama vile mbweha wa Aktiki, sungura wa mlimani, n.k.
 • Wanyama wengine wenye manyoya hukuza manyoya yao kama wakati wa baridi; hii inaboresha uwezo wa manyoya kuhifadhi joto.
 • Msimu huu huathiri pia tabia za wanyama. Kwa mfano panya kawaida huishi chini ya theluji.
 • Baadhi ya mimea ya kila mwaka haiwezi kuishi wakati wa baridi. Hata hivyo, mimea mingine ya kila mwaka inahitaji baridi kukamilisha mzunguko wa maisha yao. Baadhi ya mimea ya msimu hufaidika kwa kufunikwa na theluji wakati mimea mikubwa huacha sehemu ya juu kulala huku mizizi yake ikihifadhiwa na theluji.

Binadamu nao hufanya mambo mbalimbali ili kuweza kukabiliana na majira ya baridi.

 • Msaada wa kibinadamu hutolewa kwa mfano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi UNHCR, kama vile usambazaji wa vitu ikiwa ni pamoja na mablanketi, mafuta ya taa, mazulia ya sakafu yanayopasha nyumba joto, n.k.
 • Baadhi ya nyumba za majira ya joto, ambazo zilijengwa kwa ajili ya matumizi ya majira ya joto tu zinahitaji kutunzwa wakati wa majira ya baridi. Wakati wa msimu huu nyumba hizo hutunzwa kwa kufungwa, kuzima maji, umeme, na mistari ya simu, na kulinda vipengele mbalimbali kutokana na theluji kubwa.

Kwa mfano katika eneo la New England, nchini Marekani, familia nyingi tajiri zilizoishi humo wakati wa karne ya 19 zilikuwa na nyumba za majira ya joto milimani ili kuondoka mwanzoni mwa magonjwa kwa homa ya njano na magonjwa mengine ambayo mara nyingi yalijitokeza katika miezi ya majira ya joto.

 • Vifaa vinavyotumiwa wakati wa majira ya baridi kama vile magari, vifaa vya elektroniki, vifaa vya kilimo na umwagiliaji, boti na redio pamoja na vifaa vya kawaida huwezeshwa kutumiwa msimu huu kwa njia mbalimbali kama matumizi ya kemikali maalum.
 • Mabwawa ya samaki yanahitaji hatua kadhaa za ziada ili kuhakikisha kuwa samaki wanaishi vyema wakati wa baridi.
                                     

2. Viungovyanje

 • Jinsi ya kutunza boti
 • Hydraulic pressure in that part of the water last to freeze Archived Aprili 27, 2012 at the Wayback Machine.
 • Umuhimu wa msaada wa kibinadamu wakati wa majira ya baridi
 • Video fupi ya katuni kuhusu sababu za kuwepo kwa majira ya baridi
 • Jinsi ya kuipa nyumba joto wakati wa majira ya baridi
                                     
 • mzunguko wa majira hasa katika majira ya kuchipua baada ya majira ya baridi Tofauti na hadithi hizo, Biblia inafundisha uwezo wa Mungu juu ya kifo cha
 • ni 1  tu. Hali ya hewa ni ya kibara na ina tofauti kubwa. Majira hubadilishana kuwa na joto pia baridi kali. Wastani wa siku ni kati ya 25  C na 20  C
 • theluji ndiyo njia rahisi iliyotumiwa kufanya vinywaji kuwa baridi na wakati wa majira ya baridi mtu anaweza kuweka maziwa safi kwa muda mrefu tu kwa kuiweka
 • katika nchi zenye majira baridi mimea huanza kuotea majani mapya. Sikusare ya machipuo inakadiriwa kuwa 21 Machi kwenye nusutufe ya kaskazini na 23 Septemba
 • hiyo hakuna tofauti ya majira Tabianchi ya monsuni ya tropiki: aina hii ya tabianchi hutokea hasa Amerika Kusini na katika beseni ya Bahari Hindi ikisababishwa
 • na pia katika ukanda wa tropiki wakati wa majira ya baridi au milimani. Stroberi hupendwa sana kwa ajili ya ladha yao maalum tamu. Majani Ua Stroberi
 • Idadi inategeea na majira ni wengi wakati wa mchana na wachache wakati wa usiku. Usiku na mchana ina muda wa nusu mwaka. Macheo ya pekee hutokea kila
 • mzunguko kimenama 25 12 dhidi ya njia ya mzingo wa kuzunguka Jua. Hali hii inasababisha majira ya joto na ya baridi inayofanana na Dunia, lakini kutokana
 • kati ya sehemu ambazo ni tambarare na safu za milima. Tabianchi ni ya kibara yenye majira ya joto mafupi na majira ya baridi marefu. Sehemu kubwa ya eneo

Users also searched:

...
...
...