Back

ⓘ Malta
Malta
                                     

ⓘ Malta

Malta ni nchi ndogo kwenye funguvisiwa katikati ya bahari ya Mediteranea.

Malta iko km 93 kusini kwa kisiwa cha Sisilia Italia, upande wa mashariki kwa Tunisia na kaskazini kwa Libya.

                                     

1. Jiografia

Funguvisiwa ya Malta ina visiwa saba. Visiwa vikubwa viwili ni Malta km² 246 na Gozo km² 70. Kuna kisiwa cha tatu kinachokaliwa na watu, ndicho Comino km² 3. Vingine ni vidogo, havina watu. Jumla la eneo ni km² 316.

Visiwa vya Malta ni mabaki ya kanda la nchi kavu lililounganisha Afrika na Ulaya na kukatwa na kupanda kwa usawa wa bahari tangu mwaka 11000 KK hivi.

Sehemu za juu ni vilima vya Dingli Cliffs vyenye kimo cha mita 245 juu ya UB.

Tatizo kubwa la Malta ni uhaba wa maji baridi. Siku hizi vituo vinne vya kuondoa chumvi kwenye maji ya bahari kwa njia ya osmosi vinatengeneza maji ya kunywa. Maji machafu husafishwa na mvua kukusanywa.

                                     

2. Miji

Miji mikubwa zaidi ni: Birkirkara wakazi 21.676, Qormi wakazi 18.230, Mosta wakazi 17.789, Zabbar wakazi 15.030, Victoria wakazi 12.914 na San Gwann wakazi 12.346.

Mji mkuu Valletta una wakazi 7.173 tu.

                                     

3. Historia

Malta ilikaliwa na watu tangu milenia ya 4 KK. Kuna maghofu ya hekalu la mwaka 3200 KK hivi.

Baadaye funguvisiwa lilitawaliwa na Wafinisia, Karthago na Dola la Roma.

Malta inatajwa katika Biblia kwa sababu Mtume Paulo aliponea huko baada ya kuzama kwa merikebu alimosafiri baharini kuelekea Roma Mdo 27:39 n.k.

Waarabu walivamia visiwa hivyo mwaka 870 na kuvitawala hadi 1091.

Baadaye vilitawaliwa na Wanormandi wa Italia Kusini, baadaye tena na Wahispania chini ya mamlaka ya Dola Takatifu la Kiroma la Ujerumani.

Tangu mwaka 1530 visiwa vilikabidhiwa na Kaisari kwa askari wa Vita vya msalaba wa Chama cha Wanahospitali wa Mt. Yohane wa Yerusalemu.

Wanamisalaba hao walikuwa mabwana wa visiwa hadi Napoleoni alipoteka Malta mwaka 1799 akiwa safarini kwenda Misri.

Uingereza ulitwaa visiwa kutoka kwa Ufaransa ukatawala Malta hadi uhuru wake tarehe 21 Septemba 1964.

Tarehe 13 Desemba 1974 Malta ikatangazwa kuwa jamhuri ndani ya Jumuiya ya Madola.

Tarehe 1 Mei 2004 nchi ikajiunga na Umoja wa Ulaya.                                     

4. Watu

Kwa jumla kuna wakazi 404.039: wa kiume 200.715 49.7% na wa kike 203.324 50.3%. Msongamano wa watu ni 1.282 kwa kilomita ya mraba ambao ni msongamano mkubwa kati ya nchi zote za Ulaya.

Lugha ya Kimalta ni lugha ya pekee. Asili yake ni lahaja ya Kiarabu iliyopokea maneno mengi ya Kiitalia, Kisisili, Kiingereza, Kihispania na Kifaransa. Ni lugha pekee ya Kisemiti inayoandikwa rasmi kwa alfabeti ya Kilatini.

Lugha rasmi ya pili ni Kiingereza kutokana na miaka 150 ya ukoloni wa Uingereza. Wamalta wengi sana 66% huelewa pia lugha ya nchi kubwa jirani, Italia.

Karibu wakazi wote 98% ni Wakatoliki, na ndiyo dini rasmi ya nchi.

                                     

5. Marejeo

 • United Nations Development Programme 2006. Human Development Report 2005 – International cooperation at a crossroads: Aid, trade and security in an unequal world. Oxford University Press. ISBN 0-19-522146-X.
 • Photos of Malta. Photos of Malta. Iliwekwa mnamo 26 May 2008.
 • Jones, H. Bowen 1962. Malta Background for Development. Dhurham College. OCLC 204863.
 • Map of Malta and Gozo. Street Map of Malta and Gozo. Iliwekwa mnamo 10 April 2009.
 • 2010 Historical Dictionary of Malta. USA: Scarecrow Press, 43. ISBN 9780810853171.
 • Photos of Gozo sister island of Malta. Photos of Gozo. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-10-23. Iliwekwa mnamo 17 November 2006.
 • Charles Mifsud, The Climatological History of The Maltese Islands, Minerva 1984
 • "1942: Malta gets George Cross for bravery", BBC "On this day", 15 April 1942. Retrieved on 22 June 2006.
 • Carolyn Bain 2004. Malta. Lonely Planet Publication. ISBN 1-74059-178-X.
 • Gov.mt. Government of Malta. Iliwekwa mnamo 1 November 2005.
 • Malta. CIA World Factbook. Iliwekwa mnamo 6 September 2006.
 • Cramer, John Anthony 1828. Geographical and Historical Description of Ancient Greece. Clarendon Press, 45–46.
 • "Malta". Malta. Retrieved 1 November 2005. Archived Oktoba 28, 2009 at the Wayback Machine.
 • Paul Williams 2009. Malta – Island Under Siege. Pen and Sword Books. ISBN 978-1-84884-012-6.
                                     

6. Viungo vya nje

Serikali
 • Tovuti rasmi
 • Malta Environment and Planning Authoritys Archived Desemba 8, 2008 at the Wayback Machine. GIS
 • FinanceMalta official website
 • Laws of Malta The Official Laws of Malta website
 • The Maltese Armed Forces official website
Taarifa za jumla
 • Malta Archived Oktoba 15, 2008 at the Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
 • Malta profile from the BBC News
 • Malta Archived Novemba 24, 2020 at the Wayback Machine. – Wiki about Malta containing both general and travel related information
 • Malta entry at The World Factbook
 • Wikimedia Atlas of Malta
 • Malta katika Open Directory Project
 • Migration Malta Archived Aprili 6, 2011 at the Wayback Machine. – An information source on immigration and Malta
Vyombo vya habari
 • Malta Film Commission
 • Bartolomys photos of Malta January 2014
 • MaltaMedia – online news
 • The Times of Malta
Safari
 • Valletta Living History Official Website
 • Official Maltese Tourism website
 • Photos, Webcam of Gozo Archived Oktoba 23, 2008 at the Wayback Machine.


                                     
 • popular account of the country, its people, and its institutions including Malta and Sardinia London New York: Macmillan Co. S. Sonnenschein & Co.. 
 • ya juu zikiwemo, Foreign Extra Stout 1962 Guinness Extra Smooth 2005 Malta Guinness 1990 Harp Lager Beer 1974 Gordon s Spark 2001 Smirnoff Ice 2006
 • Nigeria. Alipata umaarufu baada ya kushinda onyesho la tatu la Amstel Malta Box Office AMBO reality show Mnamo 2009, alipokea uteuzi wa Tuzo za
 • Visiwa vya Mariana ya Kaskazini MQ Martinique MR Moritania MS Montserrat MT Malta MU Morisi MV Maldova MW Malawi MX Meksiko MY Malesia MZ Msumbiji NA Namibia
 • Jinai. Bensouda alisoma sheria nchini Nigeria na sheria za bahari nchini Malta Baada ya uasi wa kijeshi nchini Gambia wa mwaka 1994 rais mpya Yahya Jammeh
 • zinazokubali rasmi madhehebu fulani ya Ukristo: Argentina Costa Rica Liechtenstein Malta Monaco Vatican City Kitheokrasi Nyingine Andorra Dominican Republic El

Users also searched:

...
...
...