Back

ⓘ Mdudu mabawa-msuko
Mdudu mabawa-msuko
                                     

ⓘ Mdudu mabawa-msuko

Wadudu mabawa-msuko ni wadudu wadogo hadi wakubwa kiasi wa oda Plecoptera katika nusungeli Pterygota. Wadudu hawa huishi majini baridi katika muundo wa nayadi kwa muda wa mwaka mmoja hadi miaka minne kufuatana na spishi, halafu hutoka kwenye maji na kuambua na kuwa mdudu aliyekomaa wenye mabawa. Hawa ni wadudu sahili bila viungo vya kiwiliwili vilivyotoholewa. Wana viungo vya kinywa vinavyotumika kwa kutafuna, vipapasio virefu vyenye pingili nyingi, macho makubwa ya kuungwa, oseli tatu na mikia miwili mirefu. Wasiporuka wanakunja mabawa juu ya fumbatio. Nayadi wanafanana na mdudu mpevu lakini hawana mabawa na wana matamvua. Nayadi wengi zaidi hukamata arithropodi wengine wa maji, lakini nayadi wa spishi nyingine hula maada ya mimea. Wadudu wapevu hula mimea lakini wengine hawali kabisa.

Users also searched:

...
...
...